Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Wednesday, February 6, 2019

Mtuhumiwa Kesi ya Wizi wa Milioni 7 kwa dakika Asomewa Mashitaka Mapya 506

adv1
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jana imewafutia mashtaka mfanyabiashara maarufu,  Mohamed Yusufali na mwenzake Arital Maliwala.

Hata hivyo, washtakiwa hao baada ya kufutiwa kesi hiyo na kutoka katika chumba cha mahakama, walikamatwa tena na kusomewa mashitaka mapya 506
likiwamo la kuisababishia serikali hasara ya mabilioni ya shilingi, huku kesi yao ikisajiliwa kwenye Mahakama Kuu Divisheni ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, maarufu Mahakama ya Mafisadi.

Wakati hali ikiwa hiyo, upande wa Jamhuri umemuunganisha Meneja wa Benki ya I&M Tawi la Kariakoo, Sameer Khan, kwenye kesi hiyo.

Awali, Yusufali aliyedaiwa na Rais John Magufuli kuiba Sh. milioni saba kwa dakika, pamoja na mfanyakazi wake, Arifali Maliwalla, walikuwa wakikabiliwa na mashtaka 601 likiwamo kutakatisha Sh. bilioni 14.

Hata hivyo, Upande wa Jamhuri jana ulibadilisha hati ya mashtaka kutoka mashtaka 601 hadi 506 na kumuunganisha Khan katika kesi hiyo yenye namba za usajili 8/2019 na kusomwa mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Augustine Rwizile.

Katika kesi hiyo, Upande wa Jamhuri uliongozwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi Patrick Mwita akisaidiana na Mawakili wa Serikali, Esther Martin na Leornad Swai.

Wakili Mwita alidai kuwa, washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka 506, yakiwamo ya utakatishaji fedha, kuisababishia serikali hasara, kula njama, kutoa taarifa za uongo Mamlaka ya Mapato (TRA) na kughushi.
 
Baada ya kusomewa mashtaka hayo, Wakili Mwita alidai kuwa upelelezi umekamilika na wapo katika hatua ya mwisho ya kuwasilisha taarifa Mahakama Kuu Divisheni Maalum ya Uhujumu Uchumi na Rushwa.

Hakimu Rwizile alisema kesi hiyo itatajwa Februari 28, mwaka huu na washtakiwa wote wapelekwe mahabusu.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )