Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Wednesday, February 13, 2019

Muswada bima ya afya kuwasilishwa bungeni Aprili, 2019

adv1
Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema muswada wa sheria ya bima ya afya kwa wote unatarajiwa kuwasilishwa bungeni Aprili, 2019.

Ummy ameyasema hayo leo Jumatano Februari 13, 2019 katika kikao cha pamoja kati ya wizara hiyo, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa afya kutoka ndani na nje ya nchi.

Amesema lengo la Serikali ni kuwafikia Watanzania wote na kuwaingiza katika mfumo huo ili kufikia lengo la dunia namba tatu.

“Hatua ya majadiliano ndani ya Serikali imekamilika, tunatarajia kupeleka muswada bungeni mwezi Aprili,  kuwa ni lazima kwa kila Mtanzania kuwa na bima ya afya. Tukiwa na wananchi wengi waliojiunga na mifuko ya Bima ya Afya tutaweza kutoa huduma za afya kwa ufanisi zaidi,” amesema Ummy.

Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Anna Makinda amesema hatua hiyo itasaidia kuondoa maswali mengi yanaulizwa mara kwa mara na wachangiaji wa mfuko huo.

John Kadatu, akizungumza kwa kwa niaba ya mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii,  Peter Serukamba, amesema ushiriki wao katika mjadala huo wa pamoja utawasaidia kupata uelewa ili waweze kupitisha vifungu vya sheria ya masuala ya bima itakapofika bungeni.

“Tumetembelea nchi nyingi zilizofanikiwa katika mpango huu ikiwemo Ethiopia, Ghana na kwingineko tumejifunza mengi, tupo tayari kuisaidia Serikali na tuliyoyapata yatatusaidia wakati wa kupitisha vifungu kwa vifungu,” amesema Kadutu.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )