Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Saturday, February 9, 2019

Naibu Mawaziri watembelea Kituo cha kutoa huduma kwa pamoja cha Mtukula.

adv1
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Damas Ndumbaro (Mb.) amekutana na Naibu Waziri wa Masuala ya Afrika Mashariki wa Uganda, Mhe. Julius Wandera Maganda katika Kituo cha kutoa huduma kwa pamoja mpakani cha Mutukula mpakani mwa Tanzania na Uganda Tarehe 7 Februari 2019.

Mara baada ya kukutana walipata fursa ya kutembelea na kujionea namna kituo cha kutolea huduma kwa pamoja mpakani cha Mtukula (OSBP) kinavyofanya kazi na kufanya Mkutano wa pamoja uliowashirikisha wadau mbalimbali kutoka Tanzania na Uganda. Mkutano huo umefanyia Mpakani mwa Tanzania na Uganda eneo la Mtukula.

Akizungumza kwenye mkutano huo, Mhe. Dkt. Ndumbaro alisema lengo la ziara yao katika kituo hicho cha kutolea huduma kwa pamoja Mtukula ni pamoja na kujionea mafanikio na kubaini changamoto zinazokabili utendaji wa kazi na kuzipatia ufumbuzi.

Akiainisha mafanikio makubwa yaliyofikiwa na kituo hicho , Dkt. Ndumbaro alieleza namna mizigo mbalimbali ikipita kwa wakati kwa kuzingatia taratibu zote zilizopo pamoja na wafanyabiashara kati ya nchi hizi mbili wakifanya biashara zao bila vikwazo vyovyote vile.

Pamoja na mambo mengine Dkt. Ndumbaro alitumia fursa hiyo kuwajulisha wadau mbalimali waliohudhuria mkutano huo, kuwa serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, imeanzisha safari za Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL), kutoka Dar es Salaam, Arusha mpaka Enttebe, Uganda. Mafanikio hayo yametokana na mahusiano mazuri ya kidiplomasia yaliyopo baina ya Tanzania na Uganda na pia kupitia Mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Kwa upande wake Mhe Maganda, alifurahishwa na hali ya kituo hicho namna huduma zinavyotolewa. Aidha, aliahidi kuwa Serikali ya Uganda itaongeza watendaji kazi kwenye kituo hicho ili kuwezesha upande wa Uganda kufanya kazi masaa 24 kama ilivyo kwa upande Tanzania. Pia alisisitiza nchi yake kuendelea kushirikiana na Tanzania katika masuala mbalimbali ya Ushirikiano.
   
Pia katika Mkutano huo wadau walitoa pongezi kwa viongozi wa Serikali za pande zote mbili kwa kuanzisha kituo hicho cha kutolea huduma kwa pamoja mpakani Mtukula, ambapo walisema kuanzishwa kituo hicho kumeongeza chachu ya maendeleo kwa wafanyabiashara wa pande zote mbili ambapo wamekuwa wakisafirisha bidhaa zao kwa wingi bila kupata changamoto kulinganisha na hapo awali kabla ya kuanzishwa kwa kituo hicho.

 Kadhalika wadau walitoa pongezi kwa watendeji waliopo kituoni hapo kwa upande wa Tanzania, kwa kutoa huduma nzuri kwa masaa 24 kwenye kituo hicho ambapo, imepelekea wafanyabiashara kutokupoteza muda mwingi wafikapo mpakani hapo.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dodoma.
9 Februari 2019
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )