Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Sunday, February 3, 2019

Ombi la Somalia kujiunga Jumuiya ya Afrika ya Mashariki (EAC) Lasogezwa Mbele

adv1
Wakuu wa nchi za Afrika ya Mashariki (EAC), juzi walisogeza mbele hadi kikao kijacho mchakato wa Somalia kukubaliwa kujiunga na Jumuiya ya Afrika ya Mashariki (EAC) kwa mara nyingine.

Somalia iliomba kujiunga na jumuiya hiyo mwaka 2013, lakini mjadala wa ombi hilo umekuwa ukisogezwa mbele kusubiri taarifa ya watalaamu ambao watakwenda Somalia kuhakiki utayari wa nchi hiyo.

Akisoma maazimio ya mkutano wa 20 wa wakuu hao uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC), Katibu Mkuu wa EAC, Balozi Libérat Mfumukeko alisema wakuu hao pia wamelitaka Baraza la Mawaziri kukamilisha mchakato wa Sudan Kusini kushiriki katika masuala ya EAC.

Kuhusu mchakato wa kuanzishwa kwa shirikisho la kisiasa la nchi hizo, wakuu hao walimteua mshauri mwelekezi akayeandaa rasimu ya katiba ya shirikisho na kumtaka aikamilishe ndani ya miezi saba.

Mfumukeko alisema wakuu hao wa nchi wamelitaka Baraza la Mawaziri la EAC kuhakikisha siala hilo linafanyiwa kazi haraka na Rais Museveni atasaidia kutoa mwongozo.

Alisema imeamuliwa kwamba taarifa ya hatua zilizofikiwa katika mchakato wa kuanzishwa kwake itatolewa katika kikao kijacho cha 21 cha wakuu wa nchi hizo.

Katibu mkuu huyo alisema wakuu pia, wameipokea na kuikubali taarifa ya utekelezaji wa miradi ya Baraza la Mawaziri kuanzia Februari 23 hadi Januari 31.

Alisema wamelitaka baraza hilo kuendelea na utekelezaji wa kazi na miradi ya Jumuiya. Wakuu hao pia, wamepokea na kuridhia kwa kusaini itifaki kadhaa za Jumuiya na zile ambazo hazijafikiwa makubaliano, zitawasilishwa katika kikao kijacho.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )