Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Monday, February 4, 2019

Ommy Dimpoz Afunguka Baada Ya Kurejea Nchini

adv1
Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Ommy Dimpoz amerejea nchini akitokea kwenye matibabu baada ya kuugua kwa muda mrefu alipokuwa amelazwa nje ya nchi.

Akizungumza katika Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam alipokuwa amewasili Ommy Dimpoz amesema haamini kama amerudi nyumbani licha ya watu mbalimbali kumzushia kuwa amekufa.

"Hali kama unavyoiona mimi mwenyewe siamini naona nimefika nyumbani, kiukweli kuhusu uzushi wa kifo nishazoea kwa sababu ya kazi niliyoichagua inatufanya tuzoee hali kama hii.

"Lakini wanachojisahau duniani wote tunapita kila mtu atakufa na mimi nitakufa, kuhusu kuanza kuimba kwa sasa siwezi kuzungumzia chochote." amesema Ommy Dimpoz.

Msanii huyo kwa kipindi kirefu amekuwa akisumbuliwa na maradhi ya koo baada ya kusemekana kula chakula chenye sumu hali ambayo ilimfanya afanyiwe upasuaji Afrika Kusini
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )