Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Monday, February 11, 2019

Papa Francis Amteua Askofu Renatus Nkwande kuwa Askofu Mkuu Jimbo Kuu Katoliki Mwanza

adv1
Kiongozi wa Kanisa Katoliki, Papa Francis amemteua Askofu Renatus Nkwande kuwa Askofu wa Jimbo Kuu Katoliki Mwanza. 

Askofu Mkuu Mteule Nkwande alikuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Bunda tangu Februari 20, 2011.

Habari kutoka makao makuu ya kanisa hilo, Vatican zilizonukuliwa na Idhaa ya Kiswahili ya Redio Vatican, zimesema askofu Nkwande anakwenda kuziba nafasi iliyoachwa wazi, baada Papa Francis kumteua Yuda Ruwa'ichi kuwa Askofu mkuu mwandamizi katika Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Juni 21, mwaka jana.

Askofu Nkwande alipata upadri Julai 2, 1995 1995 na Novemba 27, 2010 akateuliwa na Papa Benedict XVI kuwa askofu wa kwanza wa Jimbo Katoliki la Bunda.

Aliwekwa wakfu na Kardinali Polycarp Pengo, Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Dar es Salaam, kuwa Askofu wa Bunda Februari 20, 2011.

Amepata uaskofu akiwa na miaka mitano ya upadri na uaskofu mkuu akiwa na miaka saba ya uaskofu.

Askofu mkuu mteule Nkwande alizaliwa Novemba 12, 1965, katika Parokia ya Sumve, Mwanza
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )