Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Friday, February 1, 2019

Riwaya Kali: POWER - Sehemu ya 64

adv1
MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA- 0657072588
ILIPOISHIA
       
Akanikabidhi simu yake ya kiganjani.
“Ya nini?”
“Zungumza na huyu mtu”
Nikaiweka simu yangu sikioni.
“Nashukuru sana kwa kurudi Ujerumani. Ulihisi unaweza kulikimbia ili. Tunahitaji BOKSI JEUSI haraka iwezekanavyo kabla ya hatujaharibu msiba wa mama yako”
Maneno ya mwanaume huyu yakanistua sana, jamaa huyu aliye simama eneo hili taratibu akafungua koti lake na kunionyesha bastola aliyo ichomeka kiunoni mwake akiashiria kwamba nikifanya jambo lolote la kijinga anaweza kuniua hapa hapa.

ENDELEA
Nikashusha pumzi taratibu huku nikimtazama jamaa huyu usoni mwake. Kwa ishara ya macho akaanza kunionyesha wingi wa vijana alio ambatana nao kwenye nyumba hii. Wingi wa vijana hawa wanaweza kumua mtu yoyote humu ndani.  Nikamuona Camila akija eneo nililo simama kwa kasi, jamaa huyu akaliweka sawa koti lake ili bastola yake isiweze kuonekana.
 
“Nimekuelewa, nitajitahidi kukupatia. Nipeni muda”
“Sawa sawa bwana Ethan. Tunamuona mrembo wako anakuja hapo. Angalia usije ukampoteza”
Mwnaaume huyo aliendelea kuzungumza jambo lilio nifanye nizidi kupatwa na wasiwasi.
“Sawa sawa usijali katika hilo”
Simu ikakatwa na nikamkabidhi kijana huyu na akaondoka.
“Ulikuwa unazungumza na nani mume wangu?”
“Ahaa, kuna mfanya biashara mmoja alikuwa akinipa pole sasa ametuma wawakilishi wake hapa nyumbani”
Nilizungumza huku nikiwa na wasiwasi mkubwa sana.
“Mbona kama una wasiwasi mume wangu?”
 
“Hakuna”
“Kuna hii video mume wangu. Huwezi amini kumbe yule Dany ni gaidi yule ambaye nilisha wahi kumsikia sikia kwenye historia ya magaidi wa dunia”
Camila alizungumza huku akinionyesha video hii inayo muonyesha Dany tuliye muacha nchini Tanzania na alikuwa ni msaada mkubwa sana kwetu hadi baadhi ya mazoezi amemfundisha mke wangu. Maneno ya vitisho anayo yazungumza Dany juu ya nchi ya Marekani yakaniacha mdomo wazi.
 
“Mbona hata haonekani kama ni gaidi?”
“Hata mimi mume wangu sielewi. Yaani huwezi kuamini kama ni gaidi, kuishi nasi vizuri kutusaidia kumbe ndio yule Dany halisi”
“Oooh Mungu wangu hali ya dunia inakwenda kuwa mbaya mke wangu”
“Ni kweli, sijui hili tatizo tunaweza kulitatua vipi kwa maana hii ni vita mume wangu”
Nikajikuta nikiguna huku nikimtazama Camila usoni mwake. Nikatamani kujizuia kumuambia Camila kuhusiana na vitisho ambayo nilipewa na mtu nisiye mfahamu ila nikajikuta nikizungumza tu.
“Mke wangu tuta tatizo?”
“Tatizo gani?”
“Eneo zima hili la hapa nyumbani. Limezungukwa na watu ambao wanahitaji kutuangamiza, usiangalie nyuma kwa maana wana tufwatilia”
Nilimzuia Camila kugeuza shingo yake ili kuweza kutazama watu hao walipo.
 
“Kutuangamiza kwa nini?”
“Wanahitaji boksi jeusi. Hili sekeseka la Dany na Marekani nina imani kwamba linaweza kuwasukuma watu hawa kuzidi kutushinikiza kuhakikisha kwamba tunalitoa boksi hilo jeusi”
“Ohoo Mungu wangu. Kwani boksi hilo jeusi wewe unalifahamu?”
“Sijawahi kuliona kwenye maisha yangu, ila mwanasheria alisha wahi kuniambia kwamba baba ameliacha sehemu na kuna maelekezo ambayo yapo kwenye mwili wangu na unakumbuka ulisha wahi kunichana ila ukakosa?”
 
“Ndio”
Camila alinijibu kwa unyonge kwani tukio hilo alilifanya kwa uadui mkubwa kati yangu mimi na yeye.
“Mambo ndivyo jinsi yalivyo mpenzi wangu, mimi wewe, Mery ndani huko sote hatupo salama”
“Hiyo kazi naomba uweze kuniachia mimi”
“Kazi gani?”
“Kazi ya kushuhulika na hao watu.”
“Utawafahamu vipi?”
“Dany alinifundisha uwezo mkubwa sana wa kuweza kuwafahamu maadui zangu. Nina imani kwamba nitawafahamu mmoja baada ya mwengine taratibu. Jambo la kufanya hakikisha kwamba huonyeshi wasiwasi wowote kwa mtu wa aina yoyote kwamab kuna jambo baya limepangwa kufanywa hapa nyumbani”
 
“Sawa mke wangu”
“Ngoja nijaribu basi kumtafuta Dany kama nitaweza kuzungumza naye nitamuomba aweze kusitisha mpango wake wa kwenda kuishambulia Marekani”
“Sawa mke wangu”
Camila akanibusu mdomoni kisha akaondoka eneo hili, nikarudi eneo walipo kina Frenando na nikaendelea kuzungumza nao mambo mawili matatu kisha nikachukua kombe walilo niletea na kuelekea ndani. Nikiwa ninapandisha ngazi za kuelekea gorofani, Camila akanifwata kwa nyuma na tukaingia kwa pamoja ndani huku akionekana ana habari anayo hitaji kunieleza.
“Tumewapata maadui wote”
“Wapo wangapi?”
 
“Hapa nyumbani wapo ishini na mbili”
Camila alizungumza huku akianza kunionyesha picha za watu hao. Nilamuamini sana juu ya upelelezi wake mara ya kumuona kijana ambaye amenikabidhi simu nizungumze na bosi wake.
“Eeehe tunafanyaje juu ya hawa watu?”
“Tunamuangamiza mmoja baada ya mwengine tena kimya kimya. Kisha yule kijana ndio atakuwa wamwisho yeye atatupeleka walipo wenzake”
“Hili swala inabidi uwe makini sana mpenzi wangu”
“Usijali, nina jiamini na nina uwezo mkubwa zaidi ya unavyo fikiria. Ila sijajua kwa upende wangu wewe mwenzangu”
 
“Unapnaje tukamueleza baba yako?”
“Ethan hili ni jambo la sisi wawili. Hakuna kumuambia mtu. Hapa ninasimama kama mke wako, baab yeye naye anamajukumu yake bwana”
“Nimekuelewa mke wangu”
Camila akanisogelea taratibu na kunibusu mdomoni mwanngu. Tukatazamana kwa sekunde kadhaa huku kila mmoja akisikilizia msisimko wa mwenzake. Tukaanza kunyonyana midomo yetu huku taratubu nikirudi nyuma nyuma na tukaingia bafuni kwani kufanya mapenzi katika chumba chetu kunaweza kuwafanya watu watakao pita nje ya mlango wetu kuweza kusikia kelele zetu za mahaba.
 

 

Camila alizungumza huku akikizungusha kiuno chake, unaweza kuhisi si mtoto wa Kijerumani vile na ni mswahili halisi aliye zaliwa katika kabila la wadigo ama wazaramo.
 
Tukajikuta kwa pamoja tukiimaliza safari yetu ya mapenzi, huku kila mmoja akisikilizia utamu wa viungo vyake.
“Ahaa…nilikuwa na hamu na wewe mume wangu”
“Hata mimi mke wangu”
“Sasa hapa kiu kidogo imepungua, nina imani kwamba ninaweza kwenda kufanya jambo sasa juu ya hawa washenzi”
Camila alizungumza huku  akijichomoa taratibu kwenye jogoo wangu. Akakaa kwenye choo hichi cha kukaa, akachukua toilet paper na kuanza kujifuta taratibu
 
Tulipo hakikisha kwamba viongo vyetu vipo salama. Kila mmoja akajiweka sawa nguo yake, tukatoka bafuni humu, tukajipulizia perfume kisha tukaendelea na mipango ya mazishi ya bi Jane Klopp. Wachezaji wa zamani ambao walicheza na mzee Klopp nao wakazidi kufika katika msiba huu kutoa pole ya kuondokewa na mama yetu.
 
Majira ya saa moja kasoro usiku, Camila akaniomba tuelekea kwenye moja ya chumba cha chini ya ardhi katika hii nyumba yetu. Nikaongozana naye na kuingia kwenye chumba hicho, sikuamini macho yangu mara ya kuwakuta watu wote ambao alinionyesha wakiwa wamelala chini.
 
“Umewaua hawa?”
“Hapana hakuna niliye muua. Ila kuna sumu fulani ya kisindano Dany alinifundisha nimeweza kuwashoma mmoja baada y mwengine na nimeweza kuwaleta hapa”
“Ehee huyu ndio kijana ambaye ameniletea simu yake nizungumza na bosi wake.”
“Simu yake hii hapa ninayo na nimeweza kuangalia muda ule ni nani aliweza kumpigia nimeweza kupata ni nani uliye zungumza naye”
“Ni nani?”
Camila akanionyesha picha ya mwanaume mmoja ambaye kwa haraka sana niliweza kumfahamu kwani ni miongoni mwa watu nilio kutana nao kikao cha siri nilicho fanya na viongozi wa chama cha upinzani nchini Tanzania.

==>>ITAENDELEA KESHO
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )