Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Sunday, February 10, 2019

Shirikisho La Vyama Vya Walemavu Laiomba Serikali Kupunguza Kodi

Na Farida Ramadhan, WFM, Kahama
Shirikisho la Vyama vya watu wenye ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA) wilayani Kahama, mkoani Shinyanga limeiomba Serikali kuwapunguzia kodi walemavu wenye biashara ndogo ili waweze kujikwamua kiuchumi na kuchangia uchumi wa Taifa.

Hayo yameelezwa na Katibu wa  SHIVYAWATA wilayani humo, Robert Nghomano katika semina ya elimu ya  Sera ya Taifa ya Huduma Ndogo za Fedha kwa makundi maalum iliyoandaliwa na Wizara ya Fedha na Mipango.

Alisema Serikali iangalie kwa jicho la tatu suala la kodi kwa walemavu wanaofanya biashara ndogo na ikiwezekana itoe msamaha wa kodi hizo kwani walemavu wengi wamekuwa wakifanyabiashara kwa tabu kutokana na hali zao za ulemavu.

Aidha Nghomano aliishukuru Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango kwa kutoa mafunzo ambayo yamewapa mwanga kuhusu namna ya kushiriki katika shughuli zitakazowawezesha kiuchumi na kuomba mafunzo hayo yatolewa kwa walemavu wote nchini.

Akitoa ufafanuzi katika semina hiyo , Mchumi Mkuu kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Dionisia Mjema  alisema kodi ni muhimu kwa maendeleo ya nchi, na kwa kuwa Shirikisho hilo linahitaji msamaha wa kodi waandike andiko na waliwasilishe wizarani ili waweze kusaidiwa kulingana na taratibu.

“Sasa hivi Wizara inapokea mapendekezo ya misamaha ya kodi, kama nahitaji msamaha andikeni andiko mueleze sababu za msamaha huo na Serikali itapata nini katika msamaha huo, ili kamati iangali na kujiridhisha  mtapata”, alisema.

Mjema aliongeza kuwa Serikali inatambua suala la kodi kwa wafanyabiashara wadogo ndio maana imetoa vitambulisho kwa wafanyabiashara hao maarufu kama vitambulisho vya wamachinga ambavyo vinagawiwa nchi nzima.

Naye Katibu Tarafa wa Kahama, Julias Chagama akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya hiyo aliwatoa hofu washiriki kuhusu suala la kodi na kuwaeleza kuwa katika Halimashauri ya Mji huo kunavitambulisho vingi vya wafanyabiashara wadogo  na kuwataka wajitokeze kwa wingi kuchukua vitambulisho hivyo.

Alisema Halimashauri hiyo imeandaa program mbalimbali za kuwezesha kundi maalum kiuchumi na imeshatenga Sh. Milioni 11 kwa ajili ya kundi hilo (wakiwemo walemavu) hivyo ni jukumu lao kutengeneza fursa  za kuweza kutumia fedha hizo.

Chagama alibainisha kuwa fedha hizo zitatolewa kwa mkopo usiokuwa na riba kwa vikundi vya wajasiriamali ambao tayari wameshaanza biashara ili waweze kuendeleza biashara zao.

Ameagiza watumishi wa wilaya hiyo kutoa kipaumbele kwa walemavu katika huduma mbalimbali za maendeleo ya jamii kwani nao wanahaki na wajibu wa kuchangia ukuaji wa uchumi wa nchi.

Mwisho.
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )