Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Sunday, February 10, 2019

Sumaye ahamishiwa Muhimbili, Mbowe Amtumia Salaam

Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe licha ya kuwa gerezani amemtumia salamu za pole Waziri Mkuu Mstaafu Fredrick Sumaye ambaye alipatwa maradhi ya ghafla alipokuwa mkoani Tanga.
 
Taarifa ya salamu hizo zimetolewa na chama chake ambapo amesema, "Mwenyekiti Freeman Mbowe ambaye bado yuko mahabusu Gereza la Segerea na Mbunge Esther Matiko, wamemtumia salaam za pole na kumtakia uponaji wa haraka Sumaye ili arejee katika siha njema"

Aidha taarifa ya chama hicho imeeleza kuwa Sumaye anaendelea vizuri na matibabu chini ya uangalizi wa madaktari wa Jakaya Kikwete Cardiac Institute (JKCI) alikohamishiwa baada ya kupokelewa Hospitali ya Taifa Muhimbili akitokea Hospitali ya Mkoa wa Tanga.

Aidha Katibu Mkuu wa Chama, Dkt. Vincent Mashinji, Mjumbe wa Kamati Kuu na Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa, Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa CHADEMA Patrick Ole Sosopi pamoja na viongozi wengine wa Chama ngazi na maeneo mbalimbali ya nchi, wamefika hospitalini hapo kumjulia hali.

Mzee Sumaye alipatwa na shida ya afya mapema juzi akiwa mkoani Tanga ambako alikuwa anaendelea na ratiba ya shughuli mbalimbali za Chama mkoani humo.

Kabla ya kuwasilishwa Muhimbili Sumaye alilazwa Hospitali ya Bombo kabla ya kuletwa Dar es Salaam kwa ajili ya uchunguzi zaidi wa afya yake.
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )