Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Thursday, February 28, 2019

Taarifa Kwa Umma Kuhusu Maduka Ya Kubadilisha Fedha Za Kigeni

adv1
Benki Kuu ya Tanzania ilifanya ukaguzi wa kawaida wa maduka ya kubadilisha fedha za kigeni jijini Dar es Salaam na kubaini kwamba maduka mengi yanaendesha biashara hiyo pasipo kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za utoaji wa huduma ya kubadilisha fedha za kigeni.

Kufuatia ukaguzi huo, Benki Kuu ya Tanzania imeanza utaratibu wa kufuta leseni za maduka yote yaliyokutwa yanaendesha biashara hiyo bila kuzingatia masharti ya leseni. Zoezi hili linaendelea.

Mnamo mwezi Desemba mwaka 2018, Benki Kuu ya Tanzania ilifanya ukaguzi wa maduka ya kubadilisha fedha za kigeni nchini kote na kubaini kuwa mengi hayakidhi matakwa ya kisheria ya biashara hiyo. Hivyo, iliyaandikia maduka hayo kuyataka kutoa maelezo kwa nini yasifutiwe leseni kutokana na ukiukaji huo. Hatua zilizochukuliwa jana zinatokana na tathmini ya taarifa ambazo Benki Kuu ya Tanzania ilizipokea kutoka kwa waendeshaji wa maduka hayo.

Aidha, kama ilivyoelezwa katika taarifa za Benki Kuu ya Tanzania za mwezi Novemba 2018 na tarehe 31 Januari 2019, huduma za kubadilisha fedha za kigeni zinaendelea kupatikana katika mabenki na taasisi za fedha nchini kote pamoja na maduka ya fedha za kigeni ya Shirika la Posta Tanzania (TPC).

Benki Kuu ya Tanzania inapenda kuutahadharisha umma kutotumia huduma zisizo rasmi za ubadilishaji wa fedha za kigeni kutokana na hatari mbalimbali, ikiwemo kuibiwa au kupewa fedha bandia. Aidha, utumiaji wa huduma zisizo rasmi ni kinyume cha sheria za nchi. Hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya watoaji na watumiaji wa huduma zisizo halali (black-market).

=================

adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )