Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Friday, February 8, 2019

Taarifa Ya Jeshi La Polisi Mkoani Mbeya Kuhusu Matukio Mbalimbali Yakiwemo Mauaji

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watu watatu kwa kosa la kupatikana na Pombe kali zilizopigwa marufuku nchini.

KUPATIKANA NA POMBE ZILIZOKATAZWA NCHINI.
Mnamo tarehe 07.02.2019 majira ya saa 09:00 asubuhi huko Ipyana, Kata ya Ipyana, Tarafa ya Unyakyusa, Wilaya ya Kyela na Mkoa wa Mbeya. Askari Polisi wakiwa doria walimkamata ELIZA NZIKU [19] Mkazi wa Kitongoji cha Ipyana akiuza pombe aina ya veve katoni moja iliyokatazwa kuingizwa nchini.Upelelezi unaendelea.

KUPATIKANA NA POMBE ZILIZOKATAZWA NCHINI.
Mnamo tarehe 07.02.2019 majira ya saa 10:05 asubuhi huko Kitongoji cha Isanga, Kata ya Ngonga, Tarafa ya Unyakyusa, Wilaya ya Kyela na Mkoa wa Mbeya. Askari Polisi wakiwa doria walimkamata AIDA HAMAD [19] Mkazi wa Kitongoji cha Isanga akiuza pombe zilizokatazwa kuingizwa nchini aina ya WIN katoni mbili. Upelelezi unaendelea.

KUPATIKANA NA POMBE ZILIZOKATAZWA NCHINI.
Mnamo tarehe 07.02.2019 majira ya saa 13:05 mchana huko Kyela Kati, Kata ya Kyela, Tarafa ya Unyakyusa, Wilaya ya Kyela na Mkoa wa Mbeya. Askari Polisi wakiwa doria walimkamata JAMES EMMANUEL, miaka 19, mkazi wa Kitongoji cha Mbugani akiuza pombe zilizokatazwa kuingizwa nchini aina ya WIN katoni moja. Upelelezi unaendelea.

MAUAJI – KYELA.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watu wawili 1. FRIDAY MWAMAKULA [35] Mkazi wa Njisi na 2. GOOD BOY NINGU [56] Mkazi wa Njisi kwa mahojiano zaidi kutokana na tuhuma za kuhusika kwenye tukio la mauaji ya mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la RASHID NINGO MWAMAKULA [67] Mkazi wa Kitongoji cha Njisi, Wilayani Kyela Mkoani Mbeya.

Tukio hilo limetokea Januari 08, 2019 saa 08:00 asubuhi huko Kitongoji cha Njisi kilichopo Kijiji cha Kilwa, Kata ya Kajunjumele, Tarafa ya Unyakyusa, Wilaya ya Kyela Mkoa wa Mbeya ambapo watu wasiojulikana walimvamia marehemu akiwa amelala chumbani kwake peke yake na kisha kumuua kwa kumkata na kitu kinachodhaniwa kuwa na makali/ncha kali.

Wakati wa tukio hilo mke wa marehemu aliyefahamika kwa jina la NITIKE KATETE [62] Mkazi wa Kitongoji cha Njisi alikuwa ameenda kwenye msiba wa mjukuu wake huko Kitongoji cha njisi na ndipo aliporudi alikuta mume wake ameuwawa na mwili wake ukiwa kitandani.

Inadaiwa kuwa chanzo cha tukio hilo ni mgogoro wa ardhi ya ukoo. Inadaiwa kuwa, watu hao kabla ya kutekeleza adhima yao walimvamia marehemu chumbani kwake alikokuwa amelala peke yake na kumkata kichwani kwa kitu chenye makali/ncha kali.

Mwili wa marehemu umefanyiwa uchunguzi wa kitabibu na Daktari wa Hospitali ya Wilaya ya Kyela na kukabidhiwa ndugu kwa ajili ya taratibu za mazishi. Upelelezi unaendelea kuhusiana na tukio hili.

MAUAJI – MBEYA VIJIJINI.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia Mwenyekiti wa Kijiji cha Lwanjilo anayefahamika kwa jina la STEVEN TUMPIKILE kwa ajili ya mahojiano zaidi kuhusiana na tukio la mauaji ya mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la ZAWADI JOHN @ NAMBARIWAN (Jinsia ya kiume) [35] Mkazi wa Lwanjilo.
 
Tukio hilo la mauaji limetokea Januari 07, 2019 saa 19:00 usiku huko katika kijiji na kata ya lwanjilo, Tarafa ya Tembela, Wilaya ya Mbeya Vijijini na Mkoa wa Mbeya ambapo wananchi wa Kijiji hicho waliamua kujichukulia sheria mikononi kwa kumtuhuma marehemu kuvunja nyumba ya mtu aitwaye LUFI FUNGO (Jinsia ya Kike) mchana na kuiba kitanda kimoja cha mbao ukubwa wa futi 4 kwa 5 pamoja na godoro lake na pia kuiba tena nyumbani kwa ELIZABETH SANGA debe 3 za ngano tuhuma ambazo hazikuripotiwa Polisi.

Mara baada ya wizi huo wananchi waliendesha msako wakiongozwa na wenyeviti wa vitongoji ambao ni ALIKO DAUDI @ MSEMWA na JOFREY LANGISONI ambapo katika msako huo ndipo walimkamata marehemu na vitu hivyo na kumshambulia kwa vitu vyenye ncha kali na hatimaye kufariki dunia na mwili wake kuchomwa moto.
 
Mwili wa marehemu umekutwa na majeraha makubwa kichwani na kutobolewa macho na kisha kuunguzwa kwa moto. Mwili wa marehemu umefanyiwa uchunguzi wa kitabibu na Daktari wa Hospitali Teule ya Ifisi na kukabidhiwa ndugu kwa taratibu za mazishi. Aidha msako mkali wa kuwatafuta watuhumiwa walioshuhudiwa na mama mzazi wa marehemu wakitekeleza unyama huo zinaendelea. Upelelezi unaendelea.
 
Imetolewa na:
[ULRICH O. MATEI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )