Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Friday, February 15, 2019

Taasisi Binafsi Njombe zakwepa kutumia mashine za EFD

Na Amiri kilagalila
Mamlaka ya mapato TRA mkoa wa Njombe imefanya oparesheni ya dharura ya ukaguzi wa mashine za kielektronic za kukatia risiti katika taasisi za shule , Zahanati pamoja na vituo vya afya na kubaini kuwa idadi kubwa ya taasisi hizo hazitumii mashine hizo na kutoa muda wa wiki mbili kwa taasisi hizo kununua mashine hizo vinginevyo zitapigwa faini ya kuanzia mil 3 hadi 4 kwa kuisababishia hasara serikali.

Akizungumza mara baada ya kukamilisha zoezi la ukaguzi wa mashine hizo meneja wa TRA mkoa wa Njombe Musib Shaban amesema katika uchunguzi mdogo uliofanyika wamebaini kuwa kumekuwa na ukwepaji mkubwa wa ulipaji wa mapato katika taasisi binafsi za shule na afya hali ambayo inakwamisha jitihada za serikali katika ukusanyaji wa mapato na utekelezaji wa miradi ya maendeleo .

Musibu amesema wamiliki wengi wamekuwa wakikwepa matumizi ya mashine za kielektronic kwa madai ya kukosa elimu juu matumizi ya EFD katika taasisi hizo jambo ambalo halina ukweli na kuagiza ifikapo marchi mosi kila mmiliki wa taaisisi hizo awe amenunua mashine hizo.

Wakitoa utetezi wao mara baada ya kubainika kutotumia mashine za EFD baadhi ya wamiliki na wakuu wa shule akiwemo Anna Mwalongo ambaye ni mkurugenzi wa Hagafilo Holdings pamoja na Andrew Chikwanda mkurugenzi wa GILGAL wanasema sababu kubwa ya kutotumia mashine hizo ni uelewa mdogo .

Licha ya kubainika kwamba taasisi nyingi za biashara hazitumii EFD, lakini baadhi ya watumiaji wanasema mashine hizo zimekuwa na dosari kubwa na kutoa mapendekezo kwa serikali kuhakikisha zinarekebishwa kwa wakati

Kwa mujibu wa TRA kila mfanyabaishara mwenye mauzo ya kuanzia mil 14 anapaswa kutumia EFD mashine.
tangazo
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )