Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Friday, February 1, 2019

Taasisi Za Umma Zatakiwa Kuzingatia Usalama Wa Taarifa Katika Utekelezaji Wa Serikali Mtandao

adv1
Taasisi za Umma nchini zimetakiwa kuzingatia viwango vya usalama wakati wa uundaji wa mifumo ya TEHAMA ya utoaji huduma kwa umma ili kukabiliana na changamoto ya usalama wa taarifa za serikali mitandaoni.

Wito huo umetolewa leo jijini Dodoma na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) wakati akifungua kikao kazi cha pili cha Serikali Mtandao kilichowajumuisha Watendaji Wakuu Serikalini chenye lengo la kubadilishana uzoefu, kujenga uelewa wa pamoja na kuendeleza uhusiano katika utendaji kazi na wadau mbalimbali wa Serikali Mtandao.

Mhe. Dkt. Mwanjelwa amesema kuwa, suala la usalama mitandaoni lisipokabiliwa kikamilifu, linaathiri kwa kiasi kikubwa jitihada za serikali zilizofanyika katika eneo la Serikali Mtandao na kuongeza kuwa tatizo la usalama mitandaoni linazidi kukua kadri maendeleo ya teknolojia yanavyozidi kukua.

Mhe. Dkt. Mwanjelwa amesisitiza kuwa, usalama wa taarifa za serikali liwe jambo la kwanza na la lazima wakati wa kubuni, kusanifu, kujenga, kusimika na kuendesha mifumo ya TEHAMA badala ya kujenga mifumo hiyo kwanza na ndio suala la usalama lifuate.     

“Njia mojawapo ya kuhakikisha usalama, ni kuhakikisha utengenezaji wa mifumo yetu unazingatia programu ambazo wataalamu wetu wanaweza wakatambua kinachofanyika badala ya kuwa na mifumo ambayo hatujui kinachoendelea nyuma ya pazia,” Mhe. Dkt. Mwanjelwa amesisitiza.

Mhe. Dkt. Mwanjelwa amezihimiza taasisi zote za umma kuzingatia Sheria, Kanuni, Taratibu, Viwango na Miongozo ya Serikali Mtandao iliyowekwa na inayoendelea kuwekwa ili kuhakikisha matumizi sahihi ya TEHAMA ndani ya Utumishi wa Umma.

Aidha, Mhe. Dkt. Mwanjelwa amesema, iwapo utekelezaji wa mifumo na miundombinu ya TEHAMA utawianishwa na kuwezesha ubadilishanaji wa taarifa ndani ya taasisi za umma na baina ya taasisi za umma, ni dhahiri kuwa utoaji wa huduma kwa njia ya mtandao utakuwa ni kichocheo muhimu katika kufikia maendeleo ya viwanda ambayo Serikali ya Awamu ya Tano imekusudia kuyapata.

Serikali imedhamiria kuimarisha miundo mbinu ya TEHAMA, uratibu wa shughuli za TEHAMA na usalama wa taarifa za Serikali ili kuongeza ufanisi katika sekta ya umma, kupunguza gharama za uendeshaji wa shughuli za serikali na kupanua wigo wa upatikanaji wa huduma bora kwa wananchi.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )