Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Saturday, February 16, 2019

Tazama Hapa Jinsi Juma Nature Alivyoamua Kumuaga Godzilla

Wakati wasanii wengine wakiendelea kupost katika kurasa zao za mitandao jamii na kuelezea hisia za kuguswa na kifo cha Golden Jacob 'KingZilla', hiyo imekuwa tofauti kwa mkongwe Juma Nature 'Kiroboto'.

Nature aliyewahi kutamba na ngoma kama Hakuna kulala na Sonia, yeye amemuaga Zilla kitofauti baada ya kuachia nyimbo ambayo ina ujumbe wa kumuaga msanii huyo.

Ukaribu wa wasanii hawa ulianzia pale Zilla alipomuomba Nature kufanya marudio ya wimbo wa Sonia (Remix) na kibao hiko nacho kilitamba vile vile kutokana na aina ya miondoko ya mistari ya mashairi iliyotumika katika ngoma hiyo.

Katika wimbo huu wa mwisho wa Nature alioandika maalum kwa marehemu Zilla, alisikika akiimba zaidi kwa sauti ya manung'uniko huku mstari wake wa mwisho akimalizia kwa kusema "Resting in peace my blood".

==>>Usikilize hapo chini
tangazo
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )