Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Monday, February 11, 2019

Total yazindua kiwanda cha vilainishi

Kampuni ya Mafuta ya Total Tanzania Limited, imezindua kiwanda chake cha Vilainishi (Lubricants) kilichopo katika eneo la viwanda la Chang’ombe- Temeke, Dar es Salaam.
 
Uzinduzi wa kiwanda hicho, kutaifanya kampuni ya mafuta ya
Total Tanzania kuwa ndio kampuni pekee ya kimataifa nchini Tanzania yenye kutengeneza vilainishi vyake yenyewe ambapo inatarajiwa itazalisha zaidi ya tani 15,000 za vilainishi kwa ajili ya soko la ndani ya nchi na ziada itauzwa nje nchi.
 
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kiwanda hicho uliofanyika mwishoni mwa wiki, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Joseph Kakunda, alisema kiwanda hicho cha kuchakata vilainishi vya mitambo kitasaidia nchini pamoja na kuongeza ajira.
 
“Endapo kiwanda hiki kisingejengwa, tungebaki na kiwanda kimoja cha vilainishi hapa nchini, hivyo kiwanda hicho kingezidiwa na kusababisha matokeo mabaya.
“Hivyo kiwanda hiki kitasaidia katika mambo mbalimbali. Vilainishi ni kitu muhimu na kila mtu anavitegemea, hivyo tunahitaji vilainishi vingi mara kwa mara,” alisema Kakunda.
 
Alisema nchi ya Tanzania itafaidika kwa kuokoa mamilioni ya fedha za kigeni zilizokuwa zikitumika kuagiza vilainishi, kufuatia Kampuni ya Total kujenga kiwanda cha vilainishi nchini Tanzania.
 
Alibainisha kuwa Total wamewekeza Dola milioni 20 za Marekani na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wanatarajia kupata kodi isiyopungua Dola Milioni 2 kwa mwaka (Sh. Bilioni 2.294).
 
“Kiwanda kitazalisha tani 15,000 za oili kwa mwaka, tani 750 za grisi kwa mwaka na vilainishi vya kupoza injini tani 990 kwa mwaka. Huu siyo mchango mdogo kwenye uchumi wetu ni mchango mkubwa sana,” alisema Waziri Kakunda.
 
Aidha, Waziri Kakunda alitoa wito kwa wataalamu serikalini kutambua kuwa kuna viwanda vya vilainishi Tanzania hivyo wavitumie badala ya kuagiza kutoka nje ya nchi.
 
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Total Tanzania, Tarik Moufaddal alisema kwa zaidi ya miaka 50 ya uwepo wake nchini Tanzania, Kampuni ya mafuta ya Total Tanzania ilikuwa ikiagiza vilainishi vyake kutoka nje ya nchi lakini kuanzia sasa, vilainishi hivyo vinatengenezwa hapa nchini.
 
Alisema uzinduzi wa kiwanda hicho, kutaifanya kampuni hiyo kuunga mkono kwa vitendo, mkakati wa rais Magufuli na serikali yake ya Awamu ya Tano katika ujenzi wa Tanzania ya Viwanda.
 
“Kiwanda hiki licha ya kuchangia katika maendeleo ya taifa kiuchumi na kitekinolojia, pia kitatoa nafasi za ajira kwa Watanzania,” alisema.
 
Aliongeza kuwa kupitia kiwanda hicho wamekeza dola za kimarekani Mil. 20 na wataweza kuajiri watanzania zaidi ya 100.
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )