Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Thursday, February 21, 2019

Trump achunguzwa kutaka kuiuzia teknolojia ya nyuklia Saudi Arabia

adv1
Wabunge wa Marekani wamesema wanafanya uchuguzi iwapo Rais Donald Trump anajaribu kuuza teknolojia nyeti ya nyuklia kwa Saudi Arabia, ili kuwafurahisha wafuasi wake wafanyabiashara, ambao watafaidika na mpango huo.

Bunge la Marekani tayari limeshafungua uchunguzi dhidi ya pendekezo la utawala wa Trump, la kutaka kujenga vituo kadhaa vya nyuklia nchini humo. 

Mbunge Elijah Cummings, Mwenyekiti wa Kamati ya Halmashauri ya Uangalizi na Mageuzi, ameitaka Ikulu ya Marekani kuwasilisha nyaraka za suala hilo.

Inasemekana kuwa kuna mkutano uliofanyika miezi miwili tu baada ya Trump kuingia madarakani kati ya mkwewe, Jared Kushner, na mwanamfalme Mohammed bin Salman wa Saudi Arabia , muda mchache kabla ya kutangazwa kuwa mrithi wa kiti cha ufalme wa taifa hilo.

Ripoti ya Kamati ya Uangalizi ya Baraza la Wawakilishi imesema mshauri wa zamani wa usalama wa taifa Michael Flynn na wenzake wawili ndio waliopendekeza mpango huo.

Waliuwasilisha kwa Tom Barrack, mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Sherehe ya kuapishwa kwa rais, na muungano wa kampuni za Marekani yakiongozwa na makamanda wa kijeshi waliostaafu na viongozi wa zamani wa Ikulu ya Marekani. 

Juhudi za mpango huo, ripoti imesema zilianza kabla ya Trump kuingia madarakani na kuendelea hadi baada ya kuapishwa kwake Januari 2017, licha ya wafanyakazi wa Baraza la Usalama wa Taifa kuonya kwamba uhamisho wa teknolojia ya nyuklea ya Marekani kwenda Saudi Arabia unaweza kuangaliwa kama uvunjaji wa Sheria ya Nishati ya Atomiki.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )