Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Thursday, February 14, 2019

Umoja wa Watanzania Ujerumani Wasema hawataki mkutano na viongozi wa vyama vya kisiasa

adv1
Umoja wa Watanzania waishio Ujerumani, umetoa taarifa ya kwamba hawapo tayari kujishughulisha kwa namna yoyote ya shughuli za vyama vya  kisiasa nchini Tanzania ikiwa ni pamoja na kuaanda mikutano ya wanasiasa nchini humo.

Kupitia barua iliyoandikwa na kiongozi wa umoja huo, Ephraim Makanja imeeleza mbali na kuandaa mikutano, Watanzania waishio ujerumani hawaruhusiwi kufanya mapokezi ya viongozi wa kisiasa kwa kuwa wamepata taarifa kwamba wapo wanasiasa wanataka kuwageuza jukwaa la kisiasa.

Bw. Makanja ameeleza kwamba, anawaasa watanzania wanaoishi ujerumani kutotumika kwa namna moja ama nyingine katika kuandaa mikutano ya aina hiyo na kwamba umoja huo hautakubali kutumika kama jukwaa.

"Hatutaki mkutano na viongozi wa vyama vya kisiasa kwani sisi sio kambi ya siasa," Imeeleza sehemu ya barua hiyo.

Tamko hili la Umoja wa Watanzania waishio Ujerumani limekuja kiwa ni siku chache kupita tangu Mbunge wa Singida Mashariki , Tundu Lissu alipopata nafasi ya kuzungumza Washington DC na watanzania waishio nchini Marekani.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )