Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Monday, February 11, 2019

Wabunge Wa CCM Wazungumzia Miswada Ya Sheria Iliyopitishwa Na Bunge Jijini Dodoma

Wabunge wa Chama cha Mapinduzi (CCM )leo wamekutana na waandishi wa Habari na kuzungumzia miswada sita iliyowasilishwa katika Bunge lililomalizika  huku wakionekana kufurahia zaidi mswada wa Sheria mpya ya vyama vya siasa.

Akizungumza mbele ya waandishi wa Habari Katibu wa Wabunge wa Chama cha Mapinduzi CCM Jason Rwekiza  amesema wamelazimika kuja kuzungumza na  waandishi wa Habari ili wananchi wapate kile ambacho kimefanyika Bungeni kupitia Bunge hilo.

Amesema moja ya miswaada ambayo imepitishwa na Bunge ni pamoja na miswaada wa Wakala wa maji vijijini ambao wamefanikiwa kuupitisha kwa maslahi mapana ya wananchi.

Akizungumzia kwa kirefu kuhusu mswada  wa Sheria ya vyama vya siasa Mbunge wa Jimbo la Mbinga Mjini Sixtus Mapunda alisema mswada huo ni muhimu sana kwani vyama vinaondokana kuwa vyama  vya mfukoni na kuwa Taasisi.

Mbunge Mapunda amesema  kuwa wamelazimika kulizungumzia hilo kwasababu wao ndio wenye Serikali na ndio watakaobeba lawama mwisho wasiku  na ndio maana wamejitokeza mbele ya waandishi kuzungumzia miswaada hiyo ili watanzania wajuwe kazi inayofanywa na wawakilishi wao na Serikali ya Chama cha Mapinduzi .

” Kuhusu Sheria ya vyama vya siasa inakwenda kubadili kabisa mfumo wa vyama  vya siasa Kutoka kuwa vyama vya mfukoni na kwenda kuwa taasisi kamili” alisema

Nakuongeza kuwa miaka 26 sasa tangu uwepo wa vyama Vingi wamejifunza mengi na hakuna asiyejuwa kuwa kulikuwa na malalamiko mengi juu ya matumizi ya fedha za ruzuku sasa kupitia Sheria hiyo itamfanya Mwenyekiti wa Chama kutokuwa mdhamini wa Chama husika.

Pia Mapunda alizungumzia Sheria hiyo imetoa Heshima ya kuheshimu uwepo wa mapunduzi ya Zanzibar  na pia Sheria imeleekeza nyaraka zote za vikao na maamuzi yake  kutunzwa kwa msajili wa vyama vya siasa ambaye kimsingi ndio mlezi

Aliongeza kuwa kuhusu elimu ya uraia kwa wanachama hakuna masharti na kama kuna mafunzo mengine labda kutoka nje  lazima waombe kibari Kutoka kwa msajili wa vyama vya siasa.

Kwaupande  upande wake Mbunge wa Mlalo Rashid Shangazi alisema pia yamefanyika marekebisho mbalimbali ya Sheria ikiwa pamoja na Kupandishwa hadhi kwa hifadhi na kuwa Hifadhi za taifa ambapo Tanapa wataweza kujenga Hotel na mambo mengine ya kitalii.

Alitaja baadhi Hifadhi hizo ni Hifadhi ya Biharamulo,Rumanyika,na zinginezo ambazo kwa ujumla wake zitaleta tija kwa taifa na kutoa wito kwa Tanapa  kuwekeza katika maeneo hayo.

Hata hivyo wabunge hao akiwamo Alani Kiula  Iramba Mashariki,walitolea ufafanuzi juu ya malalamiko ya madai ya kupotea kwa Fedha shilingi tirioni 1.5 na zinginezo na kusisitiza kuwa hakuna Fedha iliyopotea kwa mujibu wa taarifa ya CAG aliyowasilisha Bungeni

Alisema hata baada ya kutokea kwa hoja hizo Serikali iliagiza Ofisi ya CAG kuweza kupitia tena ukaguzi wake ili kubaini kama kuna upotevu wa fedha hizo na nyinginezo lakini bado taarifa ilionyesha hakuna upotevu hivyo wao kama wabunge wamelazimika kulitolea ufafanuzi juu ya jambo hilo.

Credit:Fullshangwe
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )