Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Friday, February 1, 2019

Wafanyakazi Wizara ya Ulinzi na JKT Watakiwa kudumisha nidhamu Kazini

adv1
Na Lazarus Masanja – wa Ulinzi
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi (Mb) amewataka Wafanyakazi wa Wizara ya Ulinzi na JKT kudumisha nidhamu na kujituma katika kufanya kazi sehemu zao za kazi.

Waziri Mwinyi ameyasema hayo alipokuwa akifungua kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa kilichofanyika katika Ukumbi wa Hazina Jijini Dodoma.

“Viongozi wote mtapimwa kwa namna mnavyofanya kazi zenu katika maeneo yenu ya kazi” alisema Dkt. Mwinyi.

Kwa upande wa viongozi Waziri Mwinyi aliwata kuwa mfano katika kufanya kazi kwa kuungoza katika ofisi zao na kuwa wabunifu kwa kushirikiana na waliochini yao pia, wafuatilie na kusimamia kazi zinazotekelezwa ili kuhakikisha malengo yaliyowekwa yanatekelezwa kwa wakati, tija na ufanisi.

Alisema, Baadhi ya viongozi huamini kuwa kukosekana kwa fedha ndiyo tatizo katika kutekeleza majukumu yao katika ofisi zao jambo ambalo sio la kweli kwani Utendaji wa kazi unahitaji mipango ambayo huandaliwa na watu  (rasilimali watu)  na rasilimali fedha hufuatia baadae.

Hivyo basi viongozi ni lazima wapange mipango yao vizuri kwa kuzingatia vipaumbele ili fedha zinapopatikana ndipo mipango itekelezwe.

Waziri pia pamoja na mambo mengine alizindua mkataba wa Wafanyakazi ambapo akasisitiza kuwa Baraza sio sehemu ya malumbano bali ni sehemu ya Wafanyakazi kutoa maoni na mapendekezo yao katika kuboresha utekelezaji kazi.

Waziri Mwinyi pia alishukuru Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwa kulidhia Muundo mpya wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa ambao umeleta mabadiliko kadhaa katika baadhi ya Idara.

Alisema, Mabadiliko hayo ni pamoja na kuunganishwa kwa Kitengo cha Milki (EMDU) na Kitengo cha Ushauri Majenzi (BCU) na kuunda Idara mpya ya Milki na Ushauri Majenzi.

Kufuatia mabadiliko hayo ya Muundo yaliyogusa pia Idara ya Utawala na Idara ya Sera na Mipango ndiyo sababu sasa Waziri anasisitiza Viongozi na Watumishi walio chini ya Idara hizo wafanye kazi kuendana ka kasi ya Serikali ya awamu ya Tano yenye kauli mbiu isemayo “Hapa Kazi tu”

Akimkaribisha Waziri wa Ulinzi na JKT ili alihutubie Baraza la Wafanyakazi, Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi Dkt. Florens Turuka amemshukuru Waziri kwa kukubali kuwafungulia Baraza na siku zote amekuwa msaada na hazina kwa Baraza hilo.

Mwenyekiti aliwatambulisha wajumbe waliohudhuria na kasha akaelezea umuhimu wa Baraza la Wafanyakazi kuwa ni kuongeza ufahamu wa pamoja wa shughuli na majukumu ya Wizara na pia kutoa ushauri katika masuala mbalimbali.

Katika hatua nyingine Baraza pia limefanya uchaguzi wa Katibu wa Baraza la Wafanyakazi ambapo Bi Illuminatha Matindi amechaguliwa kuwa Katibu wa Baraza na  Bw. Juvenary Machele Byekwasho amechaguliwa kuwa msaidizi wake.

Baada ya kufungua Baraza Mada mbalimbali zilitolewa na viongozi ambao Bw. Mchenya M John ambaye ni Katibu wa TUGHE Jiji la Dodoma na Bw. Andrew Mwalwisi ambaye ni Kamishna Msaidizi ofisi ya Kamishna Dodoma.

Kwa mujibu wa ratiba Baraza lingine linatarajiwa kufanyika kabla ya Bajeti ambalo litapitia Bajeti kabla haijasomwa Bungeni na kutoa maoni ya kufanya maboresho.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )