Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Thursday, February 14, 2019

Wambura Kuendelea Kusota Rumande....Mahakama Yagoma Kuifuta Kesi wala Kumpa Dhamana

adv1
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imesema haina mamlaka ya kumfutia kesi wala kumpa dhamana Michael Wambura baada ya Wakili wake Majura kuiomba imfutie mashitaka mteja wake kwa madai kwamba mashtaka  hayo sio ya uhujumu uchumi.

Wambura anakabiliwa na mashtaka 17 ambayo anadaiwa kuyatenda  katika ofisi za TFF, kati ya Julai mwaka 2004 na mwaka 2015

Inadaiwa kuwa Julai 7, mwaka 2004, Wambura alighushi barua akaiwasilisha TFF akijifanya barua hiyo imeandikwa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Jek System Limited ikidai malipo ya mkopo wa Dola za Marekani 30,000  zilizokopwa na TFF pamoja na riba.

Wambura anadaiwa alijipatia fedha hizo kwa nyakati tofauti na anashtakiwa kwa mashtaka mawili ya kutakatisha fedha ambapo, kati ya Agosti 15 na Oktoba 24 alitakatisha Sh 25,050,000 na 75,945,024 huku akijua fedha hizo ni zao la kosa la kughushi.


Kesi imeahirishwa hadi February 28 mwaka huu.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )