Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Monday, February 11, 2019

Wasafirishaji Dawa za Kulevya Wazidi Kubanwa.....Kamishna Jeneral Rogers Sian’ga ataka watanzania kuunganisha nguvu

adv1
Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kupambana na Kudhibiti Dawa za Kulevya Rogers Sian’ga amesema kwa sasa wamefanikiwa kidhibiti njia ambazo zilizokuwa zinatumiwa na wafanyabiashara wa dawa za kulevya kuingiza dawa hizo nchini.

Amesema kwa sasa njia ambayo inatumiwa na baadhi ya wanaojihusisha na biashara haramu ya dawa hizo imebaki ya Kusini ambako dawa zinapitishwa kutokea nchini Msumbiji na tayari wameweka mikakati ya kuidhibiti njia hiyo.

Sian’ga amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati anazungumza na waandishi wa habari kuhusu Kongamano linalotarajiwa kufanyika Februari 13 ambalo litawakutanisha wasanii wa fani mbalimbali nchini ili kujadili athari za dawa za kulevya ambapo mgeni rasmi atakuwa Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan.

Hivyo pamoja na kuzungumzia kongamano hilo, waandishi walitaka kufahamu ni kiwango gani Mamlaka hiyo imedhibiti biashara ya dawa za kulevya nchini ambapo amejibu uingizwaji wa dawa upo lakini umepungua kwa kiwango kikubwa sana ukilinganisha na miaka ya zamani kabla ya mamlaka hiyo kuwepo.

” Kwanza ifahamike kuwa usafirishaji wa dawa za kulevya sio Tanzania peke yake bali lipo katika nchi mbalimbali duniani.Tunashirikiana na nchi nyingine katika kupambana na dawa za kulevya na kuna njia ya Kusini ndio imeibuka.

“Katika mapambano hayo katika njia ya baharini mwaka jana zimekamatwa tani 9000 kutokana na ushirikiano wa nchi mbalimbali katika ukanda wa baharini.Pia mwaka jana dawa za kulevya aina ya heroin zilikamatwa kilo 185 na sehemu chache ya dawa hizo zinakwenda Msumbiji ambazo baadae zinaingizwa nchini Tanzania,” amesema.

Amefafanua kwa ujumla kiwango cha uingizwaji dawa za kulevya nchini kimepungua na kwa sasa hata wafanyabiashara wakubwa wa dawa hizo wameingia woga na kiasi wanachoingia ni kidogo ambacho ni kati ya kilo nne hadi kilo tano.”Wengi wao wanaogopa kukamatwa.”

Pia amesema dawa za kulevya aina ya Heroin na Cocaini matumizi yamepungua na hivyo dawa ambazo zinatumika ni dawa za hospitali.
 
Kuhusu kongamano la Februari 13 mwaka huu ,Kamishna Jeneral Sian’ga amsema lengo kuu ni kuhakikisha Watanzania wanaunganisha nguvu katika mapambano ya dawa za kulevya.

Hivyo kupitia kongamano hilo ambalo litawakutanisha wasanii mbalimbali nchini ambapo kupitia kongamano hilo itatolewa elimu inayohusu athari za matumizi ya dawa za kulevya, hivyo ametoa rai ya wasanii kujitokeza kwa wingi ili nao watoe maoni yao ya nini kifanyike kukomesha uingizwaji wa dawa za kulevya.

Wakati huo huo Kamishna wa Kitengo cha Kinga na Tiba wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Dk.Peter Mfisi amezungumzia umuhimu wa wasanii wa mashirikisho mbalimbali kushiriki kongamano hilo hasa kwa kuzingatia kuna baadhi ya wasanii wamekuwa wakitumia dawa za kulevya na wengine wanatumika kukubebeshwa dawa.

“Tatizo la dawa za kulevya ni la dunia nzima na wanaoatharika zaidi ni vijana wakiwamo wasanii maarufu ambao wengi wao wameathirika zaidi na wengine wamepoteza maisha kutokana na utumiaji wa dawa za kulevya.

“Si kwamba wasanii hawajui kuwa dawa za kulevya zina athari,wanajua lakini wanaangalia leo lakini ukweli athari zake ni nyingi sana.Kwa bahati mbaya wanaotumia athari zake ni kubwa. Wapo wasanii ambao wametumika kubeba dawa za kulevya kutokana na ahadi za fedha badala ya kuelezwa na matatizo yanayopatikana kupitia dawa hizo. Hivyo kupitia kongamano hilo wataeleza athari zake,” amesema Dk.Mfisi.

Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini Tanzania Joyce Fissoo ametumia nafasi hiyo kuwahamasisha wasanii wa mashirikisho mbalimbali kushiriki kongamano hilo huku akifafanua kundi ambalo linaathirika na utumiaji wa dawa za kulevya ni la wasanii.

“Tunaamini kuwa kupitia kongamano hilo ambalo mgeni rasmi atakuwa Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ,wasanii watapa fursa ya kupata elimu inayohusu athari za dawa za kulevya.Tunaomba wasanii wote wajitokeze kwa wingi na wale wa mikoani tanaomba wafuatilie kongamano hilo kupitia vyombo vya habari,”amesema Fissoo.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )