Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Wednesday, February 13, 2019

Waziri Lugola Ataka Wanaomkejeli Rais Wasakwe na Wakamatwe

Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola ameliagiza Jeshi la Polisi nchini Tanzania kushirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) kuwasaka watu wanaotoa maneno ya uchochezi dhidi ya Rais John Magufuli na Serikali.

Akizungumza na  waandishi wa habari leo Jumatatu Februari 13, 2019 jijini Arusha Lugola amesema wanaotoa maneno ya uchochezi  kupitia simu zao, Blogs na makundi ya WhatsApp watasakwa popote na kuchukuliwa hatua za kisheria.

“Watanzania tumieni vizuri mitandao ya kijamii, msitumie kuvuruga amani ya nchi, usijidanganye unaweza kufanya uchochezi na usikamatwe,” amesema akidai watu hao wanamchonganisha Rais Magufuli na wananchi.

“Kama unatoa kauli za kumtukana Rais na uchochezi ina maana kuna watu nyuma wanakutuma,” amesema Lugola.
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )