Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Saturday, February 16, 2019

Waziri Mpango Ateta Na Wafanyakazi Na Kuhimiza Maadidli Na Uwajibikaji Kazini

adv1
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango amekutana na Watumishi wa Wizara hiyo na kuzungumza nao namna bora ya utekelezaji wa  majukumu ya Wizara ili kusukuma kasi ya maendeleo ya uchumi wa Taifa.

Akizungumza katika kikao hicho Dkt. Mpango alisema Wizara ya  Fedha na Mipango ni kitovu cha Serikali hivyo  Watumishi wote wa Wizara wanawajibu wa kutekeleza majukumu kwa kuzingatia nidhamu, maadili, sheria, kanuni na  taratibu za utumishi wa Umma ili kuongeza tija.

Amesema kila mtumishi anawajibu wa kufanya kazi kwa weledi, bidii na kushirikiana na kila mmoja katika nafasi yake ili kuboresha utendaji kazi na kukuza uhusiano mahala pa kazi.

Aidha Waziri Mpango aliwapongeza Watumishi wa Wizara hiyo kwa kazi wanazozifanya hususan kazi ya uandaaji wa Bajeti Kuu ya Serikali, Uchambuzi wa Sera za Taifa na uanzishwaji wa mfumo mpya wa ukusanyaji wa mapato ya Serikali kwa njia ya Kielektroniki-GePG.

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Khatibu Kazungu amemhakikishia Waziri Mpango kuwa watatekeleza maelekezo yote aliyoyatoa kwa ukamilifu ili kuboresha utendaji kazi wa Wizara hiyo.

Mwisho.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Fedha na Mipango
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )