Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Sunday, February 10, 2019

Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi Atoa Onyo kwa Wanaomkashifu Rais

adv1
Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi amekemea tabia inayoanza kuota mzizi ya kutoa lugha zisizo za staha kwa Rais John Magufuli na kumpongeza rais kwa uvumilivu kwa lugha za adhara zinazoelekzwa kwake.

“Rais ni taswira ya nchi, hivyo si vyema kumbeza, kumdhalilisha na kumdharau tukadhani kuwa ndio demokrasia, demokrasia ni pamoja na kujua mipaka yako. Nampongeza sana Rais Magufuli kwa sababu amevumilia mengi, amevumilia upumbavu, upuuzi na ujinga mwingi”.

“Hatuna nchi nyingine zaidi ya Tanzania, si jambo jema kutumia lugha zisizo kwenye staha kwa lengo la kutafuta mabadiliko kwa kutoa lugha ya vitisho. Nchi hii inaweza kuwa na amani kama sisi wenyewe tutaamua kuwa na amani,” amesema Profesa Kabudi.

Profesa Kabudi aliyasema hayo bungeni jijini hapa juzi jioni, aihitimisha mjadala wa taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria na Katiba kuhusu kazi zake kuanzia Januari 2018 hadi Januari mwaka huu.

Naibu Waziri wa Tamisemi, Mwita Waitara amesema kitendo anachokifanya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu cha kulipaka matoke Taifa akiwa nje ya nchi, si jambo jema, ni sawa na uhaini na kusisitiza kuwa fedha zote anazotumia kuzunguka nchi mbalimbali zingeweza kusaidia wananchi wake waliomchagua.

Amesema ni vema Mbunge huyo wa upinzani akarejea nchini na kama kuna shida wazungumze, lakini hatua ya kuendelea kulipaka matope Taifa si jambo ambalo wananchi wake wamemtuma.

Mbunge wa Geita Mjini, Joseph Kasheku ‘Msukuma’ amesema pamoja na kuwa amekuwa anachambwa kwenye mitandao, anataka Lissu kutopewa mshahara na kutenguliwa uteuzi wake ili wananchi wapate mwakilishi na si anayewawakilisha kwenye televisheni.

“Waliomchagua walikuwa wanamuombea apone, na si kula bata. Sheria tumezitunga wenyewe na ni lazima tuzisimamie. Tundu Lissu si mgonjwa kwani ana uwezo wa kuzunguka katika nchi mbalimbali na kukaa kwenye ndege kwa zaidi ya saa kumi akiwa kwenye safari moja tu,” amesema mbunge huyo.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )