Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Sunday, February 17, 2019

Waziri wa Nishati Awatangazia Kiama Wakandarasi Wababaishaji

adv1
Waziri wa Nishati, Dk Medard Kalemani amesema mkandarasi anayesambaza umeme vijijini ikitokea amedanganya wananchi na serikali kwa kutotekeleza majukumu yake kadri ya makubaliano, ataadhibiwa.

Dk Kalemani aliyasema hayo akiwa wilayani Gairo mkoani Morogoro ambako alifika katika Kijiji cha Kibedya kwa ajili ya kukagua kazi ya usambazaji umeme na kutoridhishwa na kasi ya mkandarasi huyo.

“Nilipanga kuja hapa Desemba mwaka jana ndipo mkandarasi huyu akaamua kuleta umeme hapa, lakini sikuja na yeye akasimama kazi. Leo nimekuja kukagua na kukuta nyumba nyingi hazijaunganishiwa umeme na nguzo zimelala badala ya kusambazia watu nishati hii muhimu,” amesema Dk Kalemani.

Kutokana na hilo, Dk Kalemani alitoa agizo kwa mameneja wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) wa mikoa na wilaya kuhakikisha wakandarasi wa umeme vijijini wanasambaza umeme katika maeneo yote waliyopangiwa, vinginevyo mameneja hao wajiondoe kwa kushindwa kusimamia kikamilifu mradi huo.

“Ili kutekeleza mradi huu kwa kasi, naendelea kusisitiza agizo la serikali kila mkandarasi lazima awe na magenge matano ya kazi katika eneo lake ili kutorudisha nyuma juhudi za serikali za kuwasambazia umeme wananchi,” alisema Dk Kalemani.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )