Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Monday, February 4, 2019

Wema Sepetu: Sijakatwa Utumbo, Nimekonda Kisa Stress

Msanii kiwango Bongo Muvi, Wema Sepetu ameibua jipya kuhusiana na ishu yake ya kupungua uzito ambapo amesema sababu hasa iliyomfanya awe hivyo ni msongo wa mawazo ‘stress’.

Wema kwa mara ya kwanza amesema kuwa hajawahi kukata utumbo ili apungue kama watu wanavyodai, isipokuwa kipindi alichopitia kwenye lile sakata la kuvuja kwa picha zake za chumbani na Patric Christopher ‘PCK’ kilikuwa kigumu mno kwani alikuwa anapitisha hata siku tatu bila kula chochote mpaka anapepesuka.

“Watu nawashangaa sana, wanaona kukatwa utumbo ni kitu rahisi ee? Mimi nimekon­da kwa sababu ya mawazo makali niliyokuwa nayo na si vitu vingine maana nilikuwa kwenye wakati mgumu sana", amesema Wema Sepetu na kuongeza;

"Yaani hujui tu ninavyoufura­hia huu mwili wangu wa sasa, nimekuwa sio mzito tena na navaa nguo ambazo nataka na napendeza zaidi tofauti na ilivyokuwa huko nyuma, kwa kifupi najipenda hivi nilivyo".
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )