Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Thursday, March 28, 2019

Kesi ya Akina Mbowe Yakwama....Bulaya Ni Mgonjwa

adv1
Mbunge wa Bunda mjini, Esther Bulaya amesababisha kuahirishwa kwa kesi inayomkabili yeye pamoja na viongozi wengine wa juu wa CHADEMA wakiongozwa na Mwenyekiti wa Chama hicho Freeman Mbowe kutokana na kutofika mahakamani.

Leo, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ilikuwa ikisubiri mashahidi wa Upande wa Jamhuri kwa ajili ya kesi hiyo Na. 112/2018.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi 16/4/2019 kutokana na kwamba Mbunge huyo ni mgonjwa hivyo kushindwa kuhudhuria mahakamani hapo.

“Mheshiwa hakimu, Bulaya ni mgonjwa  amefanyiwa upasuaji Machi 23, 2019 katika Hospitali ya Aga Khan na kuruhusiwa kutoka hospitali hapo Machi 26, 2019, hivyo kutokana na hali yake ameshindwa kufika mahakamani hapa kusikiliza shauri hili,” amedai
mdhamini wa Bulaya, Ndeshukurwa Tungaraza

Bulaya na Viongozi wengine saba wa wa CHADEMA wanatuhumiwa kwa kosa kufanya maandamano haramu yaliyopelekea kifo cha mwanafunzi wa Akwilina, mwanzoni mwa mwaka uliopita.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )