Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Thursday, March 14, 2019

Mbowe Awashukuru Waliomsaidia Akiwa Gerezani

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Freeman Mbowe amewashukuru viongozi wa chama chake wakiwemo wabunge na wananchi ambao walijitokeza kumpigania ili kuhakikisha kiongozi huyo anatoka nje kwa dhamana.

Mbowe ametoa shukrani hizo baada ya kukaa rumande kwa zaidi ya miezi mitatu baada ya kudaiwa kukiuka  masharti ya dhamana yeye pamoja na Mbuge wa Tarime Mjini Esther.
 
Katika ujumbe huo, Mbowe ameanza kwa kusema, “Naomba niwashukuru sana wale wote walioshiriki nasi kupigana, kulia  na hata kuimarishana kwa njia mbalimbali  katika kipindi chote cha miezi mitatu na nusu tuliyoishi gerezani.”

“Natambua na kuheshimu mno ushiriki wenu kwa njia mbalimbali ikiwa ni pamoja na sala, ushauri, huduma ya chakula, michango ya fedha, solidarity support mahakamani na  zaidi walioweza kutenga muda wao na kuja kututembelea na kutufariji gerezani Segerea kulikoambatana na zawadi mbalimbali vikiwemo vitabu na magazeti, matunda, maji, juisi na hata machozi!!!.

“Nitambue kipekee kazi kubwa na ya kutukuka iliyofanywa na Mawakili Wasomi waliounda defence team yetu!! You were great all the way through!!

"Nitoe shukrani vilevile kwa wale wote waliotoa support kwa familia  zetu na hata kututunzia na kujenga kwa njia mbalimbali majimbo yetu ya uchaguzi ikiwemo kazi  ya Chadema ni Msingi.”

“Kwa wale walioshindwa vyote hivyo, watambue kwa dhati nawapenda na kuwaombea yote yaliyo mema... au kama wapo wengine waliokwazika kwa njia moja au nyingine.... pia nichukue fursa hii kuwaomba msamaha na kuitaka amani miongoni mwetu!!.

"Niwape pole nyingi wenzetu wote waliokumbwa na masahibu mbalimbali katika kipindi chote hiki!! Tuimarishwe zaidi katika mapito haya ili itimie kauli ya “kesho yetu kuwa bora kuliko jana.Mbarikiwe sana!!" Amesema Mbowe
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )