Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Sunday, March 3, 2019

Mvutano wa Rwanda na Uganda Wachukua Sura Mpya.......Mpaka Wafungwa, Rwanda Yatoa Tahadhari Kwa Raia Wake

adv1
Serikali ya Uganda imemtaka Balozi wa nchi ya Rwanda nchini humo Meja Jenerali Frank Mugambage kueleza mvutano wa kidiplomasia kuhusu sintofahamu kati ya mpaka wa nchi hizo jirani.

Uganda pia inamtaka Balozi wake nchini Rwanda kupata maelezo ni kwanini mvutano huo unaendelea kushuhudiwa.

Hali ya wasiwasi imeshuhudiwa wiki hii baada ya serikali ya Rwanda kufunga mpaka wa Gatuna kwa kile ilichosema kuwa, ulikuwa unakarabatiwa na kulazimu magari ya mizigo kutoka Uganda kupitia mpaka mwingine wa Kagitumba, umbali wa Kilomita 114.

Serikali ya Rwanda, imewataka raia wake wanaokwenda nchini Uganda kuwa makini, kwa madai kuwa raia wake wanakamatwa na kurudishwa nyumbani kwa nguvu.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )