Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Thursday, March 21, 2019

Mwigulu Nchemba Ampa Makavu Zitto Kabwe

adv1
Mbunge wa Iramba Magharbi, Dk. Mwigulu Nchemba amemjia juu Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe, kwamba hajaona utu kwenye tendo la msaada uliotolewa na serikali ya Tanzania kwa nchi tatu Malawi, Msumbiji na Zimbabwe kufuatia maafa ya kimbunga yaliyowakuta.

Mwigulu amefikia hatua hiyo baada ya Zitto kukosoa hatua ya baadhi ya wakereketwa na wafuasi wa CCM kuutangaza msaada huo huku akiweka maneno ya 'kwa hisani ya Watu wa Tanzania, jambo ambalo ameliita ni ushamba.

Dk. Mwigulu ameshangazwa na Kauli ya 'Kishamba' iliyotumiwa na Zitto ambapo amesema kauli hiyo inatumiwa na mtu anayelilia ustaarabu wakati yeye si mstaarabu, huku akihoji kwanini hajaona utu uliofanywa na badala yake ameona siasa.

"Kishamba Shamba na Kishetani?. Hii ni lugha ya mtu anayelilia ustaarabu pasipokuwa mstaarabu. Kwa utekelezaji mkubwa namna hii wa ilani ya uchaguzi ya CCM kwa jitihada za Rais?, hakuna kijiji hakijaguswa. Msaada ndio uwe wa kufanyia Siasa?", ameandika Dk. Mwigulu

adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )