Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Thursday, March 14, 2019

Profesa Lipumba Ashinda Nafasi ya Uenyekiti CUF

adv1
Mkutano mkuu wa CUF umemchagua Profesa Ibrahim Lipumba kuwa mwenyeki wa chama hicho, huku nafasi ya Maalim Seif Sharif Hamad ikiwekwa kiporo.

Akitangaza majina ya washindi katika uchaguzi huo, mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi, Thenei Ally Juma alisema jana  Machi 13, 2019 kuwa  Lipumba amepata kura 516 sawa na asilimia 88.9.

Alimtaja aliyeshinda nafasi ya Makamu Mwenyekiti Bara kuwa ni Maftaha Nachuma aliyepata kura 231 sawa na asilimia 40.9.

Juma alimtangaza pia Abbas Juma Muhunzi kuwa mshindi wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti Zanzibar baada ya kupata kura 349 sawa na asilimia 60.9.

Maalim Seif, katibu mkuu wa chama hicho amewekwa kiporo kutokana na mabadiliko ya katiba yaliyofanyika juzi ambayo yamempa nguvu mwenyekiti kuteua majina matatu ya wanachama kwa kushauriana na makamu wenyeviti wa Bara na Zanzibar.

Baada ya hatua hiyo, majina hayo yatapelekwa katika kikao cha Baraza la Uongozi ambalo litakuwa na jukumu la kumpigia kura mmoja.

Mabadiliko hayo yaliyofanywa na mkutano huo yamefuta utaratibu wa awali ambao katibu mkuu alikuwa akichaguliwa na mkutano mkuu na sasa Profesa Lipumba atakuwa ameshikilia hatima ya Maalim Seif.

Uchaguzi huo umefanyika kipindi ambacho CUF iko katika mgogoro mkubwa wa kiuongozi ulioigawa katika pande mbili - mmoja ukiwa wa Profesa Lipumba na ule wa Maalim Seif.

Mgogoro huo umekifikisha chama hicho mahakamani ambako kuna kesi kadhaa ikiwamo ya kumpinga Profesa Lipumba kuwa mwenyekiti na Machi 17, hukumu ya ama ni mwenyekiti au la itatolewa na Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )