Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Monday, April 8, 2019

Makamba: Mifuko ya Plastik Marufuku Kuanzia July 1

adv1
Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Katika kuhakikisha utunzaji wa Mazingira unaimarika hapa nchini,Serikali ina mpango wa kusitisha Matumizi ya mifuko ya  Plastiki hali ambao imekuwa tishio kubwa la uchafuzi wa Mazingira.

Hayo yamesemwa leo April 8 2019,Bungeni jiji ni Dodoma na Waziri wa  nchi,Ofisi ya Makamu wa  Rais ,Muungano na Mazingira ,Mhe.Januari Makamba wakati akijibu swali la Mbunge Wa Kaliua  Tabora Mhe.Magdalena Sakaya aliyehoji kwa kuwa Mifuko ya Plastiki imezagaa kila mahali hapa nchini,serikali ina mpango gani wa kupiga marufuku matumizi ya Mifuko hiyo.


Katika Majibu yake  Mhe.Makamba amesema serikali ina mkakati wa kupiga marufuku matumizi hayo na huenda ikasitisha kuanzia Mwezi Julai Mosi, Mwaka huu pindi taratibu zitakapokamilika.


Hata hivyo,Mhe.Makamba amesema mbadala wa matumizi ya mifuko ya  Plastiki upo na itaibua ajira nyingi kwa watanzania tofauti na ilvyo sasa mifuko ya plastiki imekuwa ikitolewa bure madukani pindi mtu anunuapo bidhaa.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )