Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Wednesday, April 17, 2019

Ofisa oparesheni mkoa wa kipolisi wa Kinondoni Atoa Ushahidi Kesi ya Freeman Mbowe na Wenzake

adv1
Ofisa oparesheni mkoa wa kipolisi wa Kinondoni ambaye  ni Mrakibu Mwandamizi wa Polisi, SSP Gerald Ngiichi ameieleza mahakama hiyo kuwa aliamuru askari kupiga risasi hewani kwa ajili ya kutawanya maandamano ya viongozi na wafuasi CHADEMA.

Ushahidi huo ambao wa kwanza kutolewa katika kesi hiyo, SSP Ngiichi alidai kuwa aliamuru risasi zipigwe kwa sababu njia ya kutumia mabomu ya Moshi ‘Machozi’ ilishindikana kuwatanya.


"Nililazimika kutumia njia ya mwisho ya kutumia silaha za moto kupigwa hewani kutoka na waandamanaji kutotii ilani tatu nilizozitoa katika umati huo wa waandamanaji kwa kutumia kingo'ra nikiwa katika gari la  polisi," alidai Ngichi.

Alidai kabla ya kutumia njia ya mwisho ya kuamuru askari wake wa vikosi vya doria kupiga risasi juu, aliamuru kikosi cha askari walikiwapo katika eneo hilo kupiga mabomu ya moshi kwa ajili ya kuwatawanya waandamanaji hao waliokuwa wanaongozwa na viongozi wa chama hicho.

Alidai wakati askari wake wakiendelea kurusha mabomu ya moshi kwa waandamanaji hao, hawakufanikiwa vizuri kutokana na moshi wa mabomu hayo kuelekea  upande walipo askari hao.

"Zoezi la  kupiga  mabomu waandamanaji hao lilikuwa  hafifu kutokana na moshi kuelekea  upande walipo askari badala ya kwenda kwa  waandamanaji kutokana na  upepo uliokuwapo eneo hilo hali iliyopelekea waandamanaji kutosambaratika" alidai Ngichi.

Alidai katika harakati za kurusha mabomu kwa waandamanaji hao,  askari polisi wawili ambao ni PC Fikiri na Koplo Rahim waliokuwapo eneo la tukio walijeruhiwa kwa mawe na kuanguka chini.

"Baada ya kuanguka chini askari hao niliamuru askari wengine watoe msaada kwa majeruhi hao kwa kuwaondoa katika eneo hilo na niliamuru kikosi cha mabomu kirudi  nyuma na kikosi cha risasi kisonge mbele ili kukabiliana na waandamanaji hao," alidai.

Alidai askari wenye silaha walisogea mbele na kupiga  risasi hewani ili kuwatawanya waandamanaji waliokiwa wanataka kuchukua silaha baada ya askari wake wawili kujeruhiwa na kuanguka chini.

"Risasi zilivyopigwa hewani kishindo kulikiwa  kikubwa hali iliyopelekea watu wengi kukimbia akiwamo mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, sikujua  kama mheshimiwa Mbowe anajua kukimbia namna hiyo," alidai Ngichi

Pia amedai, baada ya waandamanaji kusambaratika, alifanya tathmini na kubaini kuna majeruhi wawili ambapo alikuwepo Akwilina aliyewahishwa Hospitali ya Mwananyamala na baadae kuripotiwa kuwa amefariki.

Ngiichi ambaye ni Ofisa Operesheni wa Kipolisi Kinondoni, na shahidi wa kwanza wa upande wa mashitaka katika kesi ya uchochezi inayowakabili vigogo tisa wa chama hicho ameyaeleza hayo wakati akitoa ushahidi wake dhidi ya kesi hiyo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Mei 13, 14 na 15, 2019 kwa ya kuendelea kusikilizwa.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )