Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Wednesday, May 15, 2019

Kesi ya Vigogo CHADEMA: Mchomelea Vyuma atoa ushahidi Mahakamani

adv1
Shahidi wa pili katika kesi ya uchochezi inayowakabili viongozi tisa wa CHADEMA, Shaban Abdallah (19), amedai alimuona Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe akiwahamasisha wananchi kuendelea kuandamana.

Shahidi huyo ambae ni Mchomelea Vyuma anayeishi Kinondoni Moscow ameeleza hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba wakati akitoa ushahidi wake.

Shahidi Abdallah amedai Februari 16, 2018 majira ya saa 11 jioni alikuwa dukani eneo la Kinondoni Mkwajuni alisikia zogo likisogea karibu na eneo hilo ambapo aliona waandamanaji wakiwa katika hali ya shari wakiimba ‘Hatupoi mpaka mmoja afe watatuua’ ambapo alijua ni watu wa CHADEMA kutokana na mavazi yao na bendera.

Ameeleza kuwa wakati wakiendelea kuwaangalia waandamanaji hao waliona gari la polisi likiwa nyuma yao likiwatangazia watawawanyike, lakini waliendelea kulisogelea na kuanza kurusha chupa za maji na mawe..


Kesi hiyo imeahirishwa hadi Mei 15, 2019 ambapo washitakiwa wengine ni Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Salum Mwalimu,Mbunge wa Kibamba,John Mnyika,Mbunge wa Kawe,Halima Mdee,Mbunge wa Tarime Mjini,Esther Matiko,Mbunge wa Iringa Mjini,Mchungaji Peter Msigwa na Mbunge wa Tarime Vijijini,John Heche.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )