Na,Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Naibu Waziri wa Nishati,Mhe.Subira Mgalu amewataka wanachi wa Jiji la Dar Es Salaam Pamoja na Viunga Vyake kujiunga katika Group la mtandao wa kijamii wa Whatsaap ili kupata taarifa kwa uharaka juu ya katizo la Umeme .
Naibu Waziri wa Nishati,Mhe.Subira Mgalu amewataka wanachi wa Jiji la Dar Es Salaam Pamoja na Viunga Vyake kujiunga katika Group la mtandao wa kijamii wa Whatsaap ili kupata taarifa kwa uharaka juu ya katizo la Umeme .
Mhe.Mgalu amesema hayo Leo ,Mei 24,2019 bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Nyongeza la Mbunge wa Ubungo Saidy Kubenea aliyehoji pamekuwepo na katizo la Umeme katika baadhi ya maeneo mbalimbali jijini Dar E s Salaam bila wananchi kupewa taarifa na kusababisha kupata hasara katika biashara zao,nini kauli ya Serikali.
Katika Majibu Yake,Mhe.Mgalu amesema kuna Group Maalum la Whatsaap ambalo huwa linatoa taarifa kwa wakati pindi umeme unapokaribia kukatika hivyo amemtaka Mhe.Kubenea pamoja na Wananchi wake wajiorodheshe ili waunganishwe kwani Yeye alishajiunga kwenye Group hilo.
Awali,akiuliza swali la Msingi mbunge wa Kibamba John Mnyika amehoji nini ufumbuzi wa kukatika umeme mara kwa mara ,maeneo gani katika jimbo la kibamba mpaka sasa TANESCO haijafika na mkakati gani wa kupunguza gharama za umeme.
Katika Majibu yake ,Mhe.Subira Mgalu amesema tatizo la kukatika umeme katika jimbo la kibamba linatokana na zoezi la kuhamisha miundombinu ya Umeme ili kupisha upanuzi wa Barabara ya DSM-Morogoro hata hivyo tatizo hilo limepungua baada ya zoezi hilo kukamilika kwa asilimia 97 litakamilika mapema Mwezi Juni,2019.
Hata hivyo,Serikali imetenga Shilingi Bilioni 5 kwenye bajeti ya mwaka 2018/2019 kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha kupoza umeme cha Mlonganzira [Luguruni ]chenye Uwezo wa MVA 90.
Aidha,Mhe.Mgalu amesema katika maeneo ya jimbo la Kibamba ambayo hayajapatiwa Umeme ,bajeti ya Mwaka wa Fedha 2018/2019 TANESCO ilitenga
Loading...
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi
==>>... << BOFYA HAPA Kui Install>>
Mgid
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )