Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Friday, May 31, 2019

NEC yatangaza nafasi za ajira za muda za uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura

adv1
 Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetangaza nafasi za kazi za muda kwa ajili ya Uboreshaji wa Daftari la Wapiga Kura.

Kwa mujibu wa tangazo la maombi ya ajira hizo lililosainiwa na Kaimu Mkurugenzi wa Uchaguzi Mabamba Rajabu Moses, Watanzania wenye umri kuanzia miaka 18 na wasiozidi miaka 45 wametakiwa kuomba.

Sifa zingine za waombaji ni kuwa na elimu ya kidato cha nne na kuendelea na awe na ujuzi wa kutumia kompyuta.

“Awe  na uwezo wa kutambua matatizo ya kompyuta ya hardware na software an kuyatatua” ilisema sehemu ya tangazo hilo na kuongeza kuwa:.

“Awe na uwezo wa ku-istall programu za kompyuta an kutoa msaada wa kuifundi wa TEHAMA kwa watumiaji. Awe hajawahi kutiwa hatiani kwa makosa ya jinai an awe na uwezo wa kufanya kazi katika mazingira yenye usimamizi mdogo”.

Sifa nyingine za ziada za kazi hiyo zimetajwa  kwenye tangazo hilo linalopatikana kwenye Tovuti ya NEC ya www.nec.go.tz na mitandao ya kijamii ya NEC.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )