Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Wednesday, June 5, 2019

Maafisa Usalama Feki (Batili) Wanaswa Kahama Wakitapeli Mfanyabiashara

adv1
JESHI la Polisi Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga linawashikilia watu wawili kwa kujiwasilisha kuwa wao ni maafisa wa idara ya usalama wa Taifa (TSI) kwa lengo la kujipatia fedha kwa njia isiyo halali.

Watu hao ni Mrisho Zabroni (37) na Mgema Patrick (25) ambao walikwenda kwa mmoja wa wafanyabiashara wilayani hapa Abdallah Moro ambae ghala lake la kuhifadhia bidha ambalo lilifungwa na Mamala ya chakula na Dawa(TFDA)

Kwa mujibu wa kamanda wa jeshi la Polisi Mkoani Shinyanga ACP Richard Abwao amethibitisha kutokea kwa tukio hilo nakusema kuwa,watuhumiwa hao walikamatwa juzi baada ya jeshi la polisi kuwawekea mtego na kufanikiwa kuwakamata.

Amefafanua kuwa , siku ya tukio watu hao walifika kwenye ghala ya mfanyabiashara huyo na kujitambulisha kwake kuwa ni maafisa usalama wa Taifa na kumwomba rushwa kiasi cha shilingi Milioni tatu ili waweze kumsaidia kufungua ghala lake ambalo lilifungwa na TFDA.

Kamanda ABWAO amesema MORO alitoa taarifa kwa jeshi la polisi juu ya watu hao walifika kwake na kujitambulisha  kuwa wao ni maafisa usalama wa Taifa na wanauwezo wa kumfungulia ghala ambao lililokuwa limefungwa na TFDA na kumuomba fedha hizo kama Rushwa ili kufanikisha zoezi hilo.

Sanjari na hilo kamanda ABWAO amewataka wananchi na wafanyabiashara wote kuwa makini na watu wanafika kwenye biashara zao hasa maafisa ukaguzi pindi wanapofungiwa maghala yao na kujiwasilisha kwao kuwa ni maafisa usalama wa Taifa waweze kutoa taarifa ili wachukulie hatua za kisheria.

Ameongeza kuwa jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi na utakapokamilika watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma ambao zinawakabili.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )