Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Sunday, June 16, 2019

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi (CDF), Venance Mabeyo Asema dhana ya kulitegemeza Kanisa inatakiwa kufanyika kwa umakini

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi (CDF), Venance Mabeyo amesema dhana ya kulitegemeza Kanisa inatakiwa kufanyika kwa umakini ili lsiathiri shughuli za kiroho za Kanisa Katoliki.

Mabeyo ameyasema hayo leo Jumapili Juni 16, kwenye maadhimisho ya miaka 50 ya Halmashauri ya Walei iliyoongozwa na Kardinali Polycarp Pengo na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwamo Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP), Simon Sirro, Kamishna wa Uhamiaji, Anna Makakala, Spika mstaafu, Anna Makinda na Rais mstaafu wa Bunge la Afrika, Getrude Mongela.

Amesema jambo hilo liwe ni la kiimani zaidi na muumini afundishwe kwanini anatakiwa kutoa na asipotoa maana yake ni nini. Amesema hilo litasaidia kuendelea kukuza imani za waumini wa kanisa hilo kwa kufanya wanachokijua.

“Mambo haya yafanyike kwa umakini zaidi ili isionekane Kanisa linapigia chapuo mambo ya fedha kuliko imani,” amesema Mabeyo ambaye ameambatana na mkewe, Tina Mabeyo pamoja na watoto wao.

Sherehe za maadhimisho hayo zimehudhuriwa na mamia ya waumini pamoja na maaskofu wote wa Kanisa Katoliki nchini, mapadri na wawakilishi wa halmashauri za walei kutoka majimboni.
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )