Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Saturday, June 1, 2019

Serikali Yaendelea na ukarabati mkubwa wa reli ya kati inayoanzia Dar Es Salaam kwenda mikoa ya Tabora,Kigoma hadi Mwanza

adv1
Na  Christopher Philemon
Serikali imesema inafanya ukarabati mkubwa wa reli ya kati inayoanzia Dar Es Salaam kwenda mikoa ya Tabora,Kigoma hadi Mwanza ambao itagharimu takribani dola 300 za kimarekani.
 
Ukarabati huo umeanza mwaka 2018 utakamilika ifikapo mwaka 2021 na hivyo kurahisisha huduma kwa watumiaji wa usafiri huo wa gari moshi(treni).
 
Akiongea na waandishi wakati wa ziara ya kukagua ukarabati wa eneo la Kilosa hadi Itigi naibu waziri  wa Ujenzi ,uchukuzi na Mawasiliano Atashasta Nditiye,alisema kuwa ukarabati huo mkubwa unaofanywa  ili kuweza kusafirisha mizigo kutoka Dar  es Salaam kwenda nchi za jirani kama Uganda na Rwanda.
 
Nditiye alisema ukarabati huo pia utasaidia  kusafirisha abiria kwenda mikoa ya Kigoma na Tabora kwa siku mbili kutoka Dar es Salaam_kigoma ambapo itakuwa tofauti na hivi sasa gari moshi(treni)hutumia siku tatu.
 
Naibu waziri alitoa wito kwa wananchi na madereva wa magari wanaopita kukatisha reli kuwa makini kwa sababu  ukarabati huo treni itakuwa inakimbia kwa kasi ya kilometa 72 kwa saa.
 
Naye Mhandisi ,Uboreshaji wa Reli ya kati kutoka shirika la Reli Tanzania (TRC) Edwin Leonard alisema  uboreshaji wa reli hiyo unafanywa na kampuni ya China Civil Engineering Construction Corporation (CCECC)  inatekelezwa katika  vipande vinne ambayo ni Dar es Salaam- Ngerengere- Kilosa – Itigi hadi Isaka na watanzania zaidi ya elfu mbili na wageni miambili na ishirini  wamepata ajira.
 
Baadhi ya wafanyakazi wa kitanzania walioajiriwa katika kampuni hiyo walisema kuwa kazi hiyo inawasadia kupata kipato cha kuendesha maisha yao.
 
"Kwa kweli tunashukuru ukarabati huu umetupatia kazi na inatusaidia sana sisi kuweza kuendesha maisha yetuna pia tumepeleka watoto shule kwa kazi hii hii"alisema Hamisi Omary

Ukarabati wa reli hiyo unakwenda sambamba na Ujenzi wa madaraja,uinuaji wa tuta la reli  pia kujenga vituo vya kudumu vya kusimama trein pindi lifanyapo Safari zake.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )