Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Saturday, June 1, 2019

Wananchi Dodoma Wasalimisha Mifuko Ya Plastiki

adv1
Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Kufuatia katazo la matumizi ya mifuko ya plastiki lililotelewa na Waziri mkuu wa jamhuri ya muungnao wa Tanzania Mh Kasim Majaliwa wananchi jijini Dodoma wamejitokeza kusalimisha mifuko ya plastiki  katika kampuni ya usafi ya Green waste  tawi la Dodoma ambayo imefanya uzinduzi wa vituo vya kukusanya mifuko ya  plastiki.

Akizungumza katika uzinduzi wa vituo vya kupokea mifuko ya plastiki  mkurugenzi wa Halmashauri ya  Jiji la Dodoma Bwana Godwin Kunambi amesema kuwa wananchi wanatakiwa kutii sheria kwani  wameunda kamati mbalimbali ambayo itapita kila nyumba na maduka ili mifuko ya plastiki .
 
Aidha kunambi ameongeza kuwa Jiji la Dodoma limetoa elimu ya mifuko ya plastiki katika ngazi ya Mtaa,Kata,Wilaya na Taasisi zote za jiji huku akisema zipo baadhi ya taasisi zinashindwa kulipa hela ya usafi
 
Akizundua vituo vya kupokea mifuko  ya plastiki Mkuu wa Wilaya ya Dodoma  Bwana Patrobas Katambi Ambaye ndiye mgeni rasmi katika uzinduzi huo amesema kuwa wajibu wa kutunza mazingira ni jukumu la kila mwananchi ambpo amesema kuwa kwa taasisi ambazo hazilipi tozo za taka watachukuliwa sheria.

Kwa upande wake Ally Mfinanga ambaye ni Afisa Mazingira wa Jiji la Dodoma amesema kuwa kwa  atakaye bainika kuzalisha na kuingiza mifuko faini yake itakuwa ni shilingi  milioni 20.

Hatahivyo, Katambi amesema kuwa  jiji la Dodoma halitakuwa na msamaha kwa mtu yeyote atakaye kutwa na mfuko wa plastiki huku akisema kuwa watu ambao wanauza mifuko hiyo waisalimishe katika vituo ambavyo vinapokea mifuko hiyo.
 
Ikumbukwe kuwa Mwisho wa Matumizi ya Plastiki hapa nchini ilikuwa jana  Mei.31 2019 na atakayebainika anauza au kutumia mfuko wa Plastiki kuanzia  leo  Juni 1,2019 hatua kali za  kisheria zitachukuliwa dhidi yake.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )