Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Monday, July 22, 2019

January Makamba Kafunguka Tena Baada ya Mawaziri Wapya Kuapishwa

adv1
Aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, January Makamba amemshukuru Rais Dk. John Magufuli kwa kumuamini na kumteua kushika wadhifa huo.

Makamba ambaye pia ni Mbunge wa Bumbuli (CCM), uteuzi wake ulitenguliwa jana Jumapili Julai 21 na nafasi yake kuchukuliwa na aliyekuwa Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Simbachawene.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter leo Julai 22, Makamba ameandika ujumbe wa kumshukuru Rais Magufuli saa chache baada ya kuwaapisha Waziri Simbachawene na Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe ambaye amechukua nafasi ya Innocent Bashungwa aliyeteuliwa kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara.

“Neno la Mwisho kwenye hili:
Namshukuru Rais kwa kuniamini, Makamu wa Rais kwa kunielekeza, PM kwa kunisimamia, na Team ya VPO/NEMC na Mawaziri wote kwa ushirikiano. Nampongeza @HusseinBashe na Simbachawene kwa kuaminiwa. Nawatakia heri na kuwaahidi ushirikiano wangu wa dhati. 🙏🏾"
-Ameandika January Makamba

Jana Jumapili, Rais Magufuli alitangaza kutengua uteuzi wa Makamba na kumrejesha tena Simbachawene aliyewahi kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Tamisemi), miaka miwili iliyopita.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )