Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Monday, July 1, 2019

Rufaa ya Serikali Kupinga Wakurugenzi Kusimamia Uchaguzi Kusikilizwa July 30

Mahakama ya Rufani ya Tanzania imepanga kusikiliza rufaa ya Serikali ya Tanzania kupinga hukumu ya Mahakama Kuu ya Tanzania kuwaengua wakurugenzi wa halmashauri za majiji, manispaa miji/wilaya  katika usimamizi wa uchaguzi kwa niaba ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

Mahakama Kuu katika hukumu yake iliyotolewa na jopo la majaji watatu, Dk Atuganile Ngwala (kiongozi wa jopo) Dk Benhajj Masoud na Firmin Matogolo ilibatilisha kifungu cha kifungu cha 7 (1) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi kinachowapa mamlaka wakurugenzi hao kuwa wasimamizi wa uchaguzi.

Katika hukumu hiyo iliyosomwa na kiongozi wa jopo hilo la majaji waliosikiliza kesi , Dk Ngwala, mahakama hiyo ilisema kuwa kifungu hicho kinakinzana na matakwa ya Katiba ya Nchi inayotaka Tume ya Uchaguzi iwe huru.

Pia Mahakama hiyo ilibatilisha kifungu cha 7(3)  kinachoipa NEC mamlaka ya kumteua mtu yeyote miongoni mwa watumishi wa umma kuwa msimamizi wa uchaguzi, ikisema kuwa hakijabainisha namna gani kinatoa ulinzi kuhakikisha kuwa anatekeleza majukumu yake kwa uhuru.

Hata hivyo, Serikali kupitia kwa Wakili wa Serikali Mkuu, ilikata rufaa Mahakama ya Rufani kupinga sehemu ya hukumu hiyo hasa uamuzi wa kubatilisha vifungu hivyo.

Kwa mujibu wa ratiba ya vikao vya Mahakama ya Rufani vya Julai, 2019 rufaa hiyo imepangwa kusilizwa Julai 30, 2019 na jopo la Majaji watano.

Jopo la majaji hao linaongozwa na Jaji Augustine Mwarija akishirikiana na Jaji Stella Mugasha, Jaji Richard Mziray, Jaji Rehema Mkuye na Jaji Jacobs Mwambegele.

Hukumu hiyo  ya Mahakama Kuu ilitoka na kesi ya kikatiba iliyofunguliwa na watetezi na wanaharakati wa haki za binadamu na demokrasia kwa kushirikiana na vyama vya siasa, wakiwakilishwa na mwanachama wa Chama Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Bob Wangwe

Wadaiwa katika kesi hiyo namba namba 17 ya mwaka 2018 walikuwa ni  Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Mkurugenzi wa Uchaguzi.

Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )