Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Monday, August 5, 2019

CCM Kahama yawataka wananchi kuchagua viongozi waadilifu katika uchaguzi wa serikali za Mitaa.

adv1
SALVATORY NTANDU
Kuelekea katika uchanguzi wa serikali za mitaa hapa nchini wananchi wilayani kahama mkoani Shinyanga wametakiwa kuchagua viongozi bora na sio bora kiongozi ambao wataweza kusimamia fedha na miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa na serikali.

Kauli hiyo imetolewa leo na Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi wilaya ya kahama (CCM), Thomas Myonga kwenye mkutano maalum wa chama hicho wa kuwapokea wanachama sita wa Chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) uliofanyika katika kijiji cha Ufala kata ya Kilago.

Amesema katika uchanguzi wa serikali za mitaa wa mwaka huu ni vyema wananchi wakafanya maamuzi sahihi ya kuchangua viongozi wenye sifa, wasiokuwa watoa rushwa na walevi ambao sii waadilifu wanaotaka madaraka kwa maslahi yao binafsi.

Amefafanua kuwa wanachama hao sita wakiongozwa na aliyekuwa mwenyekiti wa kijiji hicho Daniel Makoye wamefanya uamuzi sahihi ya kuhamia (CCM) kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya Tano chini ya Dk John Pombe Magufuli katika kuwaletea maendeleo wananchi.

Ameongeza kuwa (CCM) mpya haina makundi hivyo ni jukumu lao kushirikiana nao katika juhudi za kuhakikisha chama hicho kinapata ushindi katika uchaguzi huo na mbinu pekee ya kushinda ni pamoja na kuweka wagombea wanaokubalika katika jamii ambao hawana sifa mbaya kama vile walevi,wazembe na wasiopenda kufanya kazi.

Myonga amewakabidhi wanachama hao wapya kadi za CCM ambao ni Daniel Makoye mwenyekiti wa kijiji cha Ufala,Bundala Busuli,Paschal Gulamali,Masanja Peter,Luhende kaswaki na Hasan Athuman ambao wote walikuwa wanachama wa CHADEMA.

Uchaguzi wa serikali za mitaa  utafanyika mwezi octoba nchi nzima.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )