Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Tuesday, August 6, 2019

Iran: Marekani inapaswa kuondoa vikwazo vyote ndo Turudi kwenye Meza ya Mazungumzo

adv1
Rais wa Iran Hassan Rouhani ameitaka Marekani iondoe vikwazo vyote dhidi ya nchi yake ikiwa inataka kufanya mazungumzo, Rais Rouhani alisema hayo alipohutubia kwa njia ya televesheni. 

Amesema hatua hiyo ni ya lazima ili mazungumzo yaweze kuendelea. 

Rais huyo amesisitiza kuwa Iran inapendelea kufanya mazungumzo lakini kwanza Marekni iondoe vikwazo vyote. Amesema lazima Iran iruhusiwe kusafirisha na kuuza mafuta yake ili mazungumzo yaendelee. 

Rais wa Iran ameeleza kuwa nchi yake ipo tayari kwa mazungumzo licha ya msimamo wa Marekani juu ya mkataba wa nyuklia uliofikiwa na nchi yake. 

Ameongeza kwamba ikiwa Marekani inataka kurudi kwenye mkataba huo ni hiari yake.

Mwaka uliopita Marekani ilijiondoa kwenye mkataba huo wa kihistoria wa kuiwekea Iran mipaka ya kurutubisha madini ya uranium ambayo ni muhimu kwa ajili ya uundaji wa silaha za nyuklia.

Iran ilisaini mkataba huo ili iondolewe vikwazo vya kiuchumi.Lakini Marekani ilisema itaongeza vikwazo dhidi ya Iran. 

Wakati huo huo wizara ya mambo ya nje ya Iran imethibitisha kwamba wajumbe wa nchi hiyo hawatahudhuria mkutano na rais Trump.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )