Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Wednesday, August 7, 2019

Msemaji Mkuu Wa Serikali Apata Kitabu Kinachoonesha Madini Yapatikanayo Nchini.

adv1
Leo tarehe Augusti 7, 2019 , Dr Hassan Abbas ambaye ni msemaji Mkuu wa serikali ya Jamhuri wa Muungano Tanzania ametembelea Banda la *GST* katika wiki ya Maonesho ya Mkutano Mkuu wa 39 wa  *SADC* kwa lengo la kupata taarifa mbalimbali za kitaalam juu ya Madini na Miamba iliyopo nchini.

Kitabu hicho ambacho ni toleo jipya  kinaonesha Madini kuanzia ngazi ya Wilaya , kata na Kijiji kimeainisha Zaidi ya madini 220.

Akiambatana na jopo la waandishi wa Habari , Dr.Hassan alipata maelezo mbalimbali kutoka kwa Mtaalam Mhandisi Priscuss Kaspana hususani katika sekta ya Madini ya viwanda yaani Industrial Minerals.

Sambamba na taarifa hizo Dr.Hassan kwa niaba ya serikali alipata zawadi ya kitabu Cha Madini Yapatikanayo Tanzania toleo jipya.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )