Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Tuesday, August 6, 2019

Mtoto wa dereva wa Mkuu wa Mkoa wa Mara aliyepata ajali afariki dunia

Mtoto wa Dereva wa Mkuu wa Mkoa wa Mara Kasobi Shida mwenye umri wa miaka 26, aliyekuwa amelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Musoma baada ya kupata ajali wakati akiendesha gari ya Mkuu wa Mkoa,Adam Malima amefariki Dunia usiku wa kuamkia leo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara Juma Ndaki amethibitisha kutokea kwa kifo hicho ambapo amesema,  kifo hicho kimetokea kwa sababu ajali aliyoipata ilikuwa ni mbaya hali iliyopelekea kijana huyo kupata majeraha ndani ya mwili wake.

''Ni kweli amefariki na sababu ya kifo chake, baada ya madaktari kumfanyia upasuaji waligundua utumbo wake umepasuka na damu imevujia ndani kwa ndani'' amesema RPC Ndaki.

Aidha Kamanda Ndaki akielezea hali ya Dereva wa Mkuu wa Mkoa (Baba wa Marehemu), amesema hali yake inaendelea vizuri na kwamba madaktari wanaendelea kumfanyia ushauri wa kisaikolojia ili arejee kwenye hali yake ya kawaida.

Kasobi Shida alipata ajali siku ya Agosti 4, baada ya kuchukua gari hilo bila ridhaa ya mzazi wake ambapo lilimshinda kuendesha na kutoka nje ya barabara kisha  kugonga daraja.
tangazo
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )