Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Thursday, August 15, 2019

Rais Cyril Ramaphosa Wa Afrika Kusini Alivyowasili Nchini Kwa Ziara Rasmi Ya Siku Mbili

adv1
Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa ameingia nchini Tanzania usiku wa kuamkia leo Alhamisi Agosti 15,2019 kwa ziara ya siku mbili kufuatia mwaliko wa Rais wa nchi hiyo, John Magufuli.

Ziara hiyo itawawezesha viongozi hao kujadili mambo yanayohusu nchi hizo, Bara la Afrika na mambo ya kimataifa na kujihakikishia wajibu wao katika ushirikiano wa karibu.

Ziara hiyo inakuja zikiwa zimebaki mbili kuelekea mkutano wa kawaida wa 39 wa viongozi wa nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) utakaofanyika jijini Dar es Salaam Agosti 17 na 18, 2019 katika ukumbi wa kimataifa wa Julius Nyerere.

Leo Alhamisi Agosti 15, 2019 saa 2: 00 atafanya mazungumzo Ikulu ya Dar es Salaam na mwenyeji wake Rais Magufuli na saa 5 hadi 8 mchana atakuwa ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) kwenye Jukwaa la Biashara.

Ijumaa ya Agosti 16, 2019 saa 3 asubuhi, Rais Ramaphosa atatembelea kambi ya wapigania uhuru Mazimbu mkoani Morogoro.


Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusine akipokewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius  Nyerere jijini Dar es salaam usiku wa kuamkia leo. Rais Ramaphosa amewasili kwa ziara rasmi ya siku mbili nchini kabla ya kuhudhuria Mkutano wa Viongozi Wakuu wa Nchi Wanachama za Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini kwa Afrika SADC
 
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )