Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Wednesday, August 7, 2019

Waziri Mkuu Aongoza Mazishi Ya Mke Wa Mwanasheria Mkuu Wa Serikali

adv1
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa leo, Agosti 7, 2019 ameongoza mazishi ya mke wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Profesa Adelardus Kilangi, Bibi Natalia Bahati Kilangi.

Akizungumza kwa niaba ya Serikali katika mazishi hayo yaliyofanyika nyumbani kwa Profesa Kilangi eneo la Luchelele jijini Mwanza, Waziri Mkuu amemuomba Profesa Kilangi na familia yake kuwa watulivu katika kipindi hiki kigumu ambapo wamempoteza mama ambaye ni nguzo muhimu ya familia.

Kadhalika, Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwasilisha salamu za pole kutoka kwa Rais Dkt. John Magufuli kwa Profesa Kilangi na familia yake kutokana na msiba mzito walioupata.

Katika salamu zake Rais Dkt. Magufuli amesema Serikali inathamini sana mchango mkubwa na mahili unaotolewa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali na anamini kwamba kwa vyovyote vile wakati wa uhai wake, marehemu Natalia alishiriki kwa kiwango kikubwa kuhakikisha kwamba mumewe anaifanya kazi yake vizuri.

Awali, Spika wa Bunge, Job Ndugai aliwasihi waombolezaji wote wamkumbuke katika sala zao, Mwanasheria Mkuu wa Seriakali Profesa Kilangi ambaye ana kazi nzito ya kuishauri Serikali na alimtaja kuwa ni kiungo muhimu cha mihimili yote mitatu.

Naye, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Mwanza, Renatus Nkwande alimuomba Profesa Kilangi na familia yake wajipe moyo kwa sababu binadamu anapokuwa hai au anapokufa bado anabaki kuwa mali ya Mwenyezi Mungu.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Umoja wa Wamiliki wa Mabenki nchini, Abdulmajid Msekela ambaye pia ni Mkurugenzi wa Benki ya CRDB alisema wanachama wote wa umoja huo wanatoa pole kwa familia na wanamwombea Mwanasheria Mkuu wa Serikali na familia nzima, Mungu awape uvumilivu katika kipindi hiki cha majonzi.

Baadhi ya viongozi waliohudhuria katika mazishi hayo ni pamoja na Waziri wa Katiba na Sheria, Balozi Augustine Mahiga, Waziri wa Madini, Doto Biteko, Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga.

Wengine ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama na Katibu Mkuu wa CCM, Bashiru Ally, Manaibu Mawazi, Wakuu wa Mikoa na wilaya na viomgozi mbalimbali wa Serikali.

Mazishi hayo pia yalihudhuriwa na Askofu wa Jimbo la Geita na Makamu wa Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania(TEC), Flavian Kassala, Mapadri na Masheikh kutoka maeneo mbalimbali nchini.

(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,        
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )