Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro, amefanya mabadiliko ya kikazi kwa Makamanda wakuu wa Mikoa minne hapa nchini.
Taarifa iliyotolewa Septemba 17 na Msemaji wa Jeshi la Polisi David Misime, imeeleza kuwa mabadiliko hayo ni ya kawaida katika uboreshaji wa utendaji wa kazi kwa jeshi hilo.
Mabadiliko hayo yamemhusisha Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro Wilbroad Mutafungwa aliyehamishiwa Makao Makuu na nafasi yake imejazwa na Hamis Issah aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro.
Makamanda wengine ni pamoja na Saidi Hamdani aliyekuwa Njombe, ambaye amehamishiwa Kilimanjaro na Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Geita, Daniel Sillah anayekwenda kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe.
Loading...
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi
==>>... << BOFYA HAPA Kui Install>>
Mgid
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )