Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Wednesday, September 18, 2019

Mohamed Dewji ‘Mo’ Alazimika kuomba Msamaha Tukio la Kutekwa na Watu Wasiojulikana

adv1
Mfanyabiashara Mohamed Dewji ‘Mo’ ameibua mjadala mtandaoni baada ya kuweka ujumbe uliowaibua wachangiaji kukumbushia tukio la kutekwa kwake.

Septemba 17, 2019 , Mo aliweka ujumbe kwenye akaunti yake ya Twitter akisema, “Kuna maisha ya mtandaoni na maisha halisi.”
 
Ujumbe huo umejadiliwa kwa mitizamo tofauti huku wengine wakikumbushia alivyotekwa na watu wasiojulikana jinsi watu walivyotumia mitandao hiyo kupaza sauti zao.

Mmoja wa watu waliojadili ujumbe huo ni mwanaharakati Maria Sarungi Tsehai alieandika “Bring Back Mo ilikuwa maisha ya mtandaoni au maisha halisi? Tutaelewana Tu”

MO Dewji baada ya kuona hivyo akaamua kuomba msamaha “Nisamehe sana dada yangu. Naona umeichukulia tweet yangu out of context. Narudia kuwashukuru wote ambao mliniombea ne kunisemea”.

Msanii Lady Jay Dee akichangia ujumbe huo amesema, “Nadhani (Mo) alimaanisha watu wanaoishi maisha ya uongo kuonyesha vitu ambavyo hawana katika maisha yao halisi. Hasa watu wengi maarufu wana hizo sana. Hata kupigia picha juice ambayo sio yako na kui post nayo ni maisha ya mtandaoni"


adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )